Wasichana waadhibiwa.

Wasichana waadhibiwa.

Under-cover

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2023
Posts
1,834
Reaction score
3,042
Korea Kaskazini inashutumiwa kuwaadhibu hadharani Wasichana wadogo na Vijana wanaotizama tamthilia au televisheni zilizopigwa marufuku Nchini humo ikiwemo televisheni za Korea Kusini, China na Mataifa ya Magharibi.

Video mpya imeonesha kundi la Wasichana wadogo akiwemo Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 akigombezwa hadharani na kukamatwa kwa kosa la hilo na Polisi wa Korea Kaskazini.

Serikali inafuatilia vikali na kudhibiti mtiririko wa habari ndani ya mipaka yake, inakataza Raia kusikiliza miziki ya kigeni, filamu na tamthilia za kigeni ambapo wanaokiuka sheria hizo hukumbana na adhabu kali ikiwa ni pamoja na kuaibishwa hadharani, kufungwa gerezani na hata kunyongwa wakati mwingine.

Vyomvo vya habari vya Korea Kusini vinaendelea kupenya Korea Kaskazini kupitia Wanaharakati wa Kusini ambao hutuma USB zilizojaa Drama na Muziki kwa kutumia maputo. #MillardAyoUPDATES
FB_IMG_1726146387516.jpg
 
Kuna mabedui wa nchi fulani wanatamani waige utawala wa Korea Kaskazini
 
Kuna mabedui wa nchi fulani wanatamani waige utawala wa Korea Kaskazini
Ila mkubwa wa kazi sawa hayo maadhabu kweli siyo ila sometimes kuna ma tamthilia ya kipumbavu mno bora hata kuyapiga stop yasioneshwe sema si unajua huyo jamaa akili zake.
 
Back
Top Bottom