Wasichana wengi wametelekezwa mitaani kama yale makontena yaliyokuwa yakisakwa

Simplicity.

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
2,636
Reaction score
1,662
Tangu shamrashamra na purkushani za kukamata majangili na wahujumu uchumi nchini zianze, hasa idara za TRA, Bandari, na Wizara kadhaa ambazo wafanyakazi wake walikuwa wanaongoza kwa kuiba, sasa mitaa mingi hasa hapa Dar, ipo kimya ajabu! Kuna wahuni walikuwa kila leo vurugu, sio baani, sio anapowasha gari kwenda kazini, sio anavyoendesha, yaani ilikuwa ni fujo nyingi na kelele mtindo mmoja.

Mtaa ulikuwa kama vile ni club na ukumbi wa starehe! Watu daily wananata huku wakiwa wameambatana na dozens za mashangingi na mademu wa mitaa lukuki! Nilikuwa najiuliza hawa watu wanafanya kazi gani mpaka wasumbue mitaa kiasi hiki?

Magufuli endelea kukaza kamba, mimi ni UKAWA in blood lakini kwa muda huu tuko pamoja, yaani mtu mshahara 675,000/= kabla haujakatwa, hana hata kibanda cha kuuza chipsi, anamiliki jumba na magari ya kifahari! Kazi tangu uanze kufanya hata miaka 2 hujafikisha! Watu tunakomaa kihalali lakini bado life tunaliona tough! Mtaa mzima ni vurugu tupu, mademu wote wako, sisi wanatupita hata salamu hupati!

Sasa nyodo zimekwisha, mademu kibao wametelekezwa mtaani, halafu kwa speed kali wanataka kutufanya sisi spare tyres! Kila leo sasa ni mwendo wa kujifanya mnanifahamu sana, mara kaka za siku nyingi? Sijui, Mbona kimya sana? Mara My upo? Mara, oh, hivi bado unaishi pale au umehama? Mara sikukuu vipi mwaka huu? Wafuate akina masamaki mkale wote sikukuu jela.

Nawaambia ile competition ya ajabu iliyokuwepo kugombania mademu kwisha, yaani ile hali akitokea tu demu mpya mtaani ananyakuliwa fasta kama vile mwewe kanyakua kifaranga cha kuku, kwishney. Mademu hasa wale grade za nyodo kwa sababu ya kuhongwa hela na vitu tulivyoibiwa na mafisadi sasa wanadoda mtaani.

Magufuli kaza kamba mpaka wakose hata hela ya bando ya kushindia JF.
 
Sasa wenye pesa halali ndiyo wanaanza kuzitumia, pesa zisizokuwa na mashaka.
 
Mbona hasira au demu wako alichukuliwa na kibopa ?
 
Kweli Mkuu tumesumbuka saana kaka mitaani uku tulikuwa hatuemi wala kueshimiwa na viela vyetu vya 20 ..30 vya kunywa bia but now tunasumbuliwa mbaya ya walewale waliotudharau ni mda wetu sasa tuacheni na sisi tupumzikee..
 
Kweli Mkuu tumesumbuka saana kaka mitaani uku tulikuwa hatuemi wala kueshimiwa na viela vyetu vya 20 ..30 vya kunywa bia but now tunasumbuliwa mbaya ya walewale waliotudharau ni mda wetu sasa tuacheni na sisi tupumzikee..

Imagine, kuna jamaa mmoja aliapa kuwa yeye kazi za serikali zenye vimishahara vya mil 3. bila marupurupu hawezi kufanya, elimu yake degree moja ya kuungaunga, anafanyia kazi TTCL, wakati kuna watanzania wanalipwa 30,000/month!
 
Kwahiyo mkuu unataka kutujuza kuwa hao mafisadi waliwekeza sana kwa wanawake badala ya maendeleo ya maana siyo? Kama ni hivyo basi Bongo tutatumia muda mrefu sana kupata maendeleo!
 
mkuu vp demu wako alichukuliwa na Mafish nini mbona una hasira nae?
 
Me kuna lishankupe limoja leo limeniomba nilitumie hata elfu 20,nimelitolea nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…