Nashangaa katika mada nyingi hawa dada ni wachangiaji wazuri sana, lakini leo mada hii nzuri inayowahusu nilitegemea kusheheni hapa lakini ni mmoja mmoja tu anaingia kama mwizi na kutoroka, wengi wanaishia kuwa visitors tu. Wao wanajua sababu zaidi kuliko sisi wanaume kwa kuwa yaliwasibu, yanawasibu na yatawasibu, vema kama wangekuja hapa tujadili ili watutoe wasiwasi na khofu tuliyo nayo.
Kuna kila dalili ya ilmu yao waipatayo inachangia kuwafanya wasijione kama wanawake bali wamejiweka mahali fulani ambapo si pao kwa vile hawawezi kufikia pale kwa wanaume kwa vile siyo nature yao. Kwa maana hiyo kuendelea kuwa mahali amapo si pako utaonekana kama kichokoo tu.
Ilmu kwa mategemeo yangu yaweza msidia zaidi mwanake kujikomboa kwa maana ya kutambua haki zake katika jamii na kuzienzi badala ya kutoka kwenye hulka yake na kujiweka pasipohusika na hatima yake kuonekana si pake na kukwepwa na wanaume, matokeo yake anabaki kuwa chombo cha kuridhia wengi badala ya heshima ya mwenzi wa maisha yanye kumlindia heshima na utu wake.
Kwamba elimu waliyopata inawafungua akili na kuamua kubaki walivyo bila kuolewa kwa ridhaa yao ni hoja dhaifu, maana kuna kitu kinachofichwa hapo na kuegemea tu kutoa hitimisho ambalo ni matokeo ya udhaifu fulani wanaokuwa nao hawa akina dada wasomi. Wanaume wasomi wengi tu wanachamgamkia kuoa licha ya umri wao kuwa umepita, ingawa hii kwa wanaume haileti athari binafsi kukosa wa kumwoa hata kama mwanaume umri umeingia hatua ya umakamu.
Dalili za wazi ni msichana ajiweke na kuonekana ni msichana, mwenye hulka ya kiusichana, mwenye mtazamo wa kusikilizana asijiweke juu ya kichwa cha mtazamiwa wake, ambaye anaonekana kulinda haki na kupenda utamaduni wetu ambao mambo yake ni mazuri na mabaya kutoyaruhusu kwa malengo ya kujenga familia bora.
Mitindo ya wasichana wasomi kupendelea mambo ya viigizo vya kwenye net work ambavyo ni asili yake kubuniwa na wafanya biashara hizo ili kutunza misuli yao kuwawezeswha kufanya shughuli za biashara kwa muda mrefu kumewazodoa wengi na kujikuta pengine kuogopwa na wanaume wengi. Maana utembezaji wa bidhaa hizo za kimachinga mwanaume anaogopa kuchakaza kandambili nyingi kwa siku moja kutokana na mizunguko isiyoisha ya kuzungukia kupata vitumbua au mapambizo ya pilau anayotaka. Yaliyo mbele hayaoni kama yanafaa ingawa yanaweza kufanya pilau ipendeza na kutoa harufu nzuri tu kwa kutumia hizi nazi za kukunwa tulizozoea tangu utotoni na mababu zetu walitumia hawakupungukiwa na kitu.
Kwa vyo vyote kuna mengi, ila cha msingi tungemweka Mungu mbele ya macho yetu na kujikuta tunatembea mbele ya macho ya Mungu yanayotuangalia kila saa nadhani tungejenga na kuridhia yale ambayo Muumba anatuandalia, vinginevyo yapekee tuyatakayo katu hayataturidhia maana dhana ya binadamu ni hii ya kila zaidi apatavyo ndivyo atamanivyo, na hatima ni kuishia kuhangaika maisha yote bila kuamua moja na kuridhia hakuna kutulia, maana ya kuamua kubaki peke ndiyo nzuri na katika uzani madhara ni makubwa wakati fulani kuliko unafuu tunaofikiria.