Wasifu/Biography wa Ali Masoud (Masoud Kipanya)

vampire_hunter007

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
1,034
Reaction score
2,624
Huyu jamaa nimekuwa nikimfuatilia muda mrefu.. Aisee huyu jamaa ni kichwa sana.. Yaani unaweza ukachukua threads kibao za JF na comments za watu, lakini yeye akaweza kuyapresent kwa mchoro mmoja tu..

Matatizo mengi sana ya kijamii amekuwa akiyawakilisha katika michoro yake.. Na kuna muda inahitaji akili ya ziada kuweza kuelewa michoro yake.. Michoro yake mingi imejaa Sarcasm na inakosoa kila penye kosa bila kujali ni upande wa serikali wala upinzani..

Kuna muda anaweza akatoa mchoro wake ukauchukulia poa mpaka baada ya muda ndo unaelewa alichokimaanisha.. Mfano ile ishu ya Sefue kutumbuliwa..

Nikawaza kuwa huyu jamaa anapaswa kupewa degree ya heshima na vyuo vyetu hapa Tz..

Hebu mwenye kumjua vizuri historia yake kielimu aitupie hapa ili tumfahamu kwa undani... Jamaa ni kichwa sana..

================

 
Ni moja kati ya role model wangu wa Kitanzania coz of creativeness na uthubutu alionao kufanya kila anachofikiri anaweza refer to vipindi vyake vya maisha plus na kile kipindi kilichokua tbc akiwa anageuza pori kuwa kijiji
 
Masoud Kipanya ni kichwa sana. Hata ukimsikiliza akiongea "ujinga" nyuma yake kuna shule. Kuna siku aliwahi kumuita Waziri mmoja mpuuzi kwenye kipindi cha PB enzi hizo ....ile kusawazisha mambo akamuuliza Fina Mango .."hivi mpuuzi ni mtu wa namna gani? Mpuuzi si mtu anayepuuzia mambo?" ...[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
 
Nashangaa siku hizi anasjida kubwa usoni!Wakati ameanza kusali ukubwani tu..kitu kinanishangaza sana..watu waliozaliwa Saudi Arabia au Dubai ..ambao huwa wameanza kusali toka wakiwa wadogo hawana sijda, lakini wabongo ambao wameijua dini ukubwani,wanasugua uso makusudi mpaka itokee sijda ili waonekane ni watu wadini.Ajabu sana...
 

Watu wanaulizia CV wewe unakuja na sijda...kumfuatilia mtu kiasi hicho ni dalili za uchawi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…