Wasifu wa Julius Nyerere: Combined Dancing Club Tabora 1945

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
WASIFU WA JULIUS NYERERE: COMBINED DANCING CLUB TABORA 1945

Katika Wasifu wa Julius Nyerere mwandishi kaeleza uhusiano wa Mwalimu Nyerere na Maulidi Kivuruga mmoja wa wanachama wa Combined Club, Tabora na jinsi Maulidi Kivuruga alivyomshauri Nyerere wafungue duka la ushirika la TAA na duka likafunguliwa.

Hii ilikuwa mwaka wa 1947.

Katika kitabu cha Abdul Sykes nimemweleza Maulidi Kivuruga vipi yeye na wenzake akiwapo ndugu yake Abdallah Kivuruga walivyounda African Association mwaka wa 1945:

''Tabora ilianza kushiriki katika siasa mwaka 1945 wakati African Association ilipoingizwa mjini Tabora kutoka Dodoma kutokana na juhudi za Edward Mwangosi.

Tabora kwenyewe msukumo wa katika kuanzisha chama cha Waafrika zilitoka kutoka Combine Dancing Club, kilabu kilichoanzishwa na vijana wa pale mjini kwa ajili ya kujifurahisha. Wanachama mashuhuri wa kilabu hiyo walikuwa ndugu wawili Wamanyema - Maulid na Abdallah Kivuruga, Chamngíanda Usingizi, Ramadhani Nasibu, Rashid Mussa, Issa Kibira, Hamis Wabeba, Mwinyi Khatib Hemed, Swedi Juma, Issa Hamis Pama na Rajab Kanyama. Kumbukumbu za kikoloni zinaonyesha kwamba kamati ndogo ndani ya kilabu iliundwa katika mwaka 1945, Mwinyi Khatibu Hemed, Mzigua kutoka Bweni, Pangani, akiwa katibu. Hemed aliandika barua makao makuu ya African Association mjini Dar es Salaam kuujulisha uongozi juu ya dhamira ya kufungua tawi mjini Tabora.

Tarehe 3 Machi, 1945 African Association mjini Tabora ilifungua ofisi yake ikiwa na na viongozi wafuatao: Hamisi Simbe (Rais), Ramadhani Nasibu (Makamu wa Rais), M. K. Hemed (katibu), Chamngíanda Usingizi (Mwenyekiti), Fimbo Mtwana (Mweka Hazina) na Rashidi Mussa (Mkaguzi wa Hesabu).''

Picha: Kulia ni Abdallah Kivuruga na kushoto ni Maulidi Kivuruga.
 
WASIFU WA JULIUS NYERERE: COMBINED DANCING CLUB TABORA 1945

Katika Wasifu wa Julius Nyerere mwandishi kaeleza uhusiano wa Mwalimu Nyerere na Maulidi Kivuruga mmoja wa wanachama wa Combined Club, Tabora na jinsi Maulidi Kivuruga alivyomshauri Nyerere wafungue duka la ushirika la TAA na duka likafunguliwa.

Hii ilikuwa mwaka wa 1947.

Katika kitabu cha Abdul Sykes nimemweleza Maulidi Kivuruga vipi yeye na wenzake akiwapo ndugu yake Abdallah Kivuruga walivyounda African Association mwaka wa 1945:

''Tabora ilianza kushiriki katika siasa mwaka 1945 wakati African Association ilipoingizwa mjini Tabora kutoka Dodoma kutokana na juhudi za Edward Mwangosi.

Tabora kwenyewe msukumo wa katika kuanzisha chama cha Waafrika zilitoka kutoka Combine Dancing Club, kilabu kilichoanzishwa na vijana wa pale mjini kwa ajili ya kujifurahisha. Wanachama mashuhuri wa kilabu hiyo walikuwa ndugu wawili Wamanyema - Maulid na Abdallah Kivuruga, Chamngíanda Usingizi, Ramadhani Nasibu, Rashid Mussa, Issa Kibira, Hamis Wabeba, Mwinyi Khatib Hemed, Swedi Juma, Issa Hamis Pama na Rajab Kanyama. Kumbukumbu za kikoloni zinaonyesha kwamba kamati ndogo ndani ya kilabu iliundwa katika mwaka 1945, Mwinyi Khatibu Hemed, Mzigua kutoka Bweni, Pangani, akiwa katibu. Hemed aliandika barua makao makuu ya African Association mjini Dar es Salaam kuujulisha uongozi juu ya dhamira ya kufungua tawi mjini Tabora.

Tarehe 3 Machi, 1945 African Association mjini Tabora ilifungua ofisi yake ikiwa na na viongozi wafuatao: Hamisi Simbe (Rais), Ramadhani Nasibu (Makamu wa Rais), M. K. Hemed (katibu), Chamngíanda Usingizi (Mwenyekiti), Fimbo Mtwana (Mweka Hazina) na Rashidi Mussa (Mkaguzi wa Hesabu).

Juhudi za kuihuisha TANU zilikuja mwaka 1955 mwaka mmoja baada ya TANU kuasisiwa Dar es Salaam kupitia Young New Strong Football Club - club ya kandanda iliyoanzishwa miaka mingi nyuma ambayo ilikuwa maarufu pale mjini.

Wanachama wa club hiyo baadhi yao ndiyo walikuwa waasisi wa African Association, mashuhuri miongoni mwao walikuwa Fundi Mhindi na Maulidi Kivuruga.

Mwenyekiti wa kilabu hiyo alikuwa Juma Mrisho, mcheza kandanda mashuhuri kwa siku zile.
Shaaban Mohamed Silabu na Bilali Rehani Waikela walikuwa Katibu na Naibu Katibu.
Picha: Kulia ni Abdallah Kivuruga, kushoto ni Maulidi Kivuruga na Bilal Rehani Waikela."

Picha: Kulia ni Abdallah Kivuruga, kushoto ni Maulidi Kivuruga na picha ya chini ni Bilal Rehani Waikela.

Angalia picha:
Screenshot_20200611-000627.jpg
 
Attachments

  • BILAL REHANI WAIKELA.jpg
    BILAL REHANI WAIKELA.jpg
    29.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom