Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
WASIFU WA JULIUS NYERERE: MIKUTANO YA TANU JANGWANI 1950s
Bibi Titi Mohamed yuko pembeni kwa Julius Nyerere juu ya jukwaa dogo la miti.
Angalia hizo nyumba nyuma ya Nyerere hivyo ndivyo Kariakoo ya miaka hiyo ilivyokuwa.
Angalia umati wa watu waliokuja kuwasikiliza Nyerere na Bibi Titi.
Angalia baraghashia za wenyeji wa Mzizima zilivyoupamba mkutano wa TANU.
Waandishi wanasema mikutano ya TANU ya mwanzo ilikuwa inakosa watu.
Hili sikupatapo kulisikia.
Daisy Sykes katika kumbukumbu ya miaka 50 ya kifo cha baba yake ameandika katika makala yake, "Abdulwahid Sykes I Knew," kuwa siku moja kabla ya mkutano Julius Nyerere, Dossa Aziz na viongozi wengine walikuwa wakikutana nyumbani kwao na baba yake Bwana Abdul alikuwa anapanga vipi akina mama watakuja uwanjani.
Mipango hii ilifanikiwa sana kuwahamasisha wake kwa waume kuhudhuria mikutano ya TANU.