Wasimamizi na waangalizi wa mitihani hawataruhusiwa kubeba simu zao za mkononi katika vyumba vya mitihani

Wasimamizi na waangalizi wa mitihani hawataruhusiwa kubeba simu zao za mkononi katika vyumba vya mitihani

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Wizara ya Elimu ya Kenya, kupitia Baraza la Kitaifa la Mitihani la Kenya (KNEC), imeanzisha sheria mpya za usimamizi wa mitihani ya KCSE (Mitihani ya taifa ya shule ya msingi) na KPSEA (Mitihani ya taifa ya shule ya sekondari) kwa mwaka 2024.

Miongoni mwa sheria hizo ni kwamba wasimamizi na waangalizi wa mitihani hawataruhusiwa kubeba simu zao za mkononi katika vyumba vya mitihani, huku majina ya watahiniwa yakipangwa kuchapishwa moja kwa moja kwenye karatasi zao za mitihani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mitihani hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa KNEC, David Njengere, alisema kuwa jumla ya watahiniwa 2,279,414 watakaa kwa mitihani hiyo mwaka huu. Watahiniwa wa KCSE ni 965,501 katika vituo 10,565 na watahiniwa wa KPSEA ni 1,303,913 katika vituo 35,573.

"Mwaka huu, tumeimarisha usalama wa vifaa vya mitihani kwa kuongeza makontena 41 mapya, na hivyo kufikia jumla ya makontena 617 yatakayotumika kuhifadhi na kusafirisha vifaa vya mitihani kwa usalama," alisema Njengere.

Waziri wa Elimu, Julius Migos, alionya vikali wale watakaojihusisha na udanganyifu au makosa yoyote ya mitihani, akisema kuwa serikali haitakuwa na huruma kwa yeyote atakayepatikana akijihusisha na udanganyifu huo.

"Serikali haitakuwa na huruma kwa yeyote atakayekamatwa akihusika na makosa ya mitihani," alisema Migos.

Mkurugenzi wa Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC), Antoninah Lentoinjoni, alibainisha kuwa wasimamizi wa mitihani watahamishwa kutoka vituo walivyokuwa wakisimamia awali, ili kuhakikisha usimamizi wa haki.

"Hakuna mtu atakayepangiwa kusimamia mitihani kwenye kituo ambacho ana maslahi ya moja kwa moja," alisema Lentoinjoni.

USSR
 
Mjifunze Tz kwenye chumba cha mtihani simu yoyote hairuhusiwi kwa mtu yeyote ni miaka mingi sana
 
Back
Top Bottom