LGE2024 Wasimamizi Serikali za Mitaa 2024 wanapatikanaje?

LGE2024 Wasimamizi Serikali za Mitaa 2024 wanapatikanaje?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
4,035
Reaction score
11,462
Huu uchaguzi umeanza kwa wasimamizi kupigiwa simu badala ya kutoa Matangazo ya watu kutuma maombi ya kusimamia uchaguzi huo. Hii inaleta picha kuwa Serikali kupitia TAMISEMI imeamua kuharibu tena uchaguzi kwa makusudi.

Haya mambo siyo ya kufumbia macho kabisa Serikali fuateni utaratibu hawa watumishi mnaowapigia simu wakasimamie zoezi hili bila kutuma maombi watasimamia kwa uweledi kweli zoezi hili nyeti kuelekea uchaguzi mkuu?
 
Acha uongo mkuu, mm nafanya biashara zangu huku Mwanza, mbona Tangazo lilibandikwa Kwenye Ofisi ya Katibu Kata nadhan wanamuita Mtendaji Kata sijui Afisa Mtendaji Kata...
 
Acha uongo mkuu, mm nafanya biashara zangu huku Mwanza, mbona Tangazo lilibandikwa Kwenye Ofisi ya Katibu Kata nadhan wanamuita Mtendaji Kata sijui Afisa Mtendaji Kata...
Kata gani na halimashauri ipi
 
Leta ushahidi wa mtu hata mmoja aliyepigiwa simu bila yeye kuomba kuwa msimamizi wa uchaguzi.
Bila ushahidi huu ni uzushi na kuweweseka na kutafuta visingizio. Burden of proof ipo kwa aliyeleta haya madai.
 
Ushahidi Gani mkuu? Uliza utaambiwa
 
Chichiem wanausimamia huo uchaguzi mwanzo mwisho

Ova
 
Ushahidi Gani mkuu? Uliza utaambiwa
Ndio nimeuliza leta huo ushahidi
Watu waliopigiwa simu wakiwa hawajaomba hiyo kazi ya usimamizi.Kama huna ushahidi basi withdraw hilo andiko lako.
 
Ndio nimeuliza leta huo ushahidi
Watu waliopigiwa simu wakiwa hawajaomba hiyo kazi ya usimamizi.Kama huna ushahidi basi withdraw hilo andiko lako.
Siwezi kufuta na ushahidi ninao
 
Back
Top Bottom