Uchaguzi 2020 Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutengua uteuzi wa Wagombea Udiwani utasababisha uchaguzi wa Madiwani wengi kubatilishwa na Mahakama

Matojo Cosatta

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2017
Posts
234
Reaction score
390
UAMUZI WA MWISHO WA KUTENGUA UTEUZI WA MADIWANI ULIOFANYWA WA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI UTASABABISHA UCHAGUZI WA MADIWANI KUTENGULIWA NA MAHAKAMA.

Karibu maamuzi yote ya Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi (Assistant Returning Officers) kutengua uteuzi wa wagombea udiwani wa vyama vya siasa katika Uchaguzi Mkuu huu wa 2020 utasababisha uchaguzi wa madiwani wengi sana takribani asilimia zaidi ya 90% au hata 100% kubatilishwa na Mahakama kwa makadirio yangu kutokana na sampling ambayo nimefanya kuhusu utenguaji wa uteuzi wa wagombea udiwani kwa sababu uamuzi wa mwisho (final decisions) karibu wote (au hata wote) wa kutengua uteuzi wa wagombea udiwani kupitia mapingamizi umefanywa na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi badala ya Wasimamizi wa Uchaguzi (Returning Officers) kama inavyotaka sheria ya uchaguzi.


Uamuzi wa Msimamizi Msaadizi wa Uchaguzi kutengua uteuzi wa wagombea udiwani kupitia mapingamizi sio wa mwisho badala yake ni uamuzi wa kimapendekezo ( recommendatory decision) kwa maana ya kwamba Msimamizi Msaadizi wa Uchaguzi anatoa mapendekozo kwa Msimamizi wa Uchaguzi ama kutengua au kutotengua uteuzi wa mgombea udiwani na Msimamizi wa Uchaguzi pekee ndo ana mamlaka ya kutengua uteuzi wa mgombea diwani ama kwa kukataa (refusal) au kukubaliana (approval) na mapendekezo ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 28 (5) ya Kanuni za Uchaguzi wa Mamlaka za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani), 2020 (Tangazo la Serikali Na. 401 la 2020).

The decision of Assistant Returning Officer with regards to disqualification of a candidate for the office of councillor is not a final decision rather it is a mere recomendatory or advisory decision which is subject to mandatory review and approval of Returning Officer under provisions of Regulation 28 (5) of the Local Authorities (Councillors' Elections) Regulations, 2020 ( G.N. No. 401 of 2020).

Kitendo cha Msimamizi Msaadizi wa Uchaguzi kufanya uamuzi wa mwisho (final decision) wa kutengua uteuzi wa wagombea udiwani kupitia mapingamizi ni kinyume na sheria na ni uvunjaji wa wazi wa masharti ya Kanuni ya 28 (5) ya Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani, 2020.

Hivyo basi, uvunjifu huu wa sheria ni mojawapo ya sababu ambayo inatosha kabisa kubatilisha uchaguzi wa diwani wa kata husika kwa kuwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi amevuka mipaka ya mamlaka yake (unlawful assumption of power) na katika mazingira haya Kunga ya Utila Vayasi (Doctrine of Ultra Vires) itaingilia kati kutoa adhabu ya kubatilisha uchaguzi kutokana na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kuvuka mipaka ya mamlaka yake ya kisheria. To this end, Doctrine of Ultra Vires is expected to come into play to penalise excess of jurisdiction or unlawful assumption of statutory power by Assistant Returning Officers.

Pia, uamuzi wa kutengua uteuzi wa diwani kupitia mapingamizi lazima uandikwe na Msimamizi wa Uchaguzi (Returning Officer) kwa mujibu wa Kanuni ya 28 (6) ya Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani, 2020 na sio Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.

Maamuzi mengi kama sio yote ya kutengua uteuzi wa wagombea udiwani yameandikwa na kusainiwa na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzini kitendo ambacho ni kinyume na sheria na ni uvunjaji wa wazi wa masharti ya Kanuni ya 28 (6) ya Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani, 2020.

Authored by Electoral Law Fitnaologist based in Dar es Salaam.
 
Mahakama hizi za CCM kamwe haziwezi kutenda haki, zimewekwa MFUKONI na jiwe siku nyingi. Tuombe Mungu serikali hii ya WATEKA NYARA ifurumushwe kupitia uchaguzi Mkuu, iwe kwa kura ama MAANDAMANO YASIYO NA KIKOMO.
 
Hahaha hakuna kupita bila kupingwa, mechi lazima ichezwe.
 
Mahakama hizi za CCM kamwe haziwezi kutenda haki, zimewekwa MFUKONI na jiwe siku nyingi. Tuombe Mungu serikali hii ya WATEKA NYARA ifurumushwe kupitia uchaguzi Mkuu, iwe kwa kura ama MAANDAMANO YASIYO NA KIKOMO.

Hii hoja ya ultra vires iko wazi sana bila shaka yoyote hata mwanafunzi wa sheria wa mwaka wa 3 anajua hiki kitu, hivyo, sitarajii kama mahakama inaweza kutoa uamuzi tofauti na kubatilisha uchaguzi wa diwani ambaye ameshinda uchaguzi baada ya uteuzi mgombea mwenzake kutenguliwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.
 
Leo tume ya uchaguzi imekubali rufaa 15 za wagombea.
Je, ni hizo tu au bado ni muendelezo? But take from me kuna makapi yametuuza kwa makusudi kujaza form. Bahati nchi hii sio Colombia, wasaliti wangepewa pipi zao.
 
Ingekuwa ni mahakama za Kenya ningekuelewa.
 

Hii mbona hatari.
 
Mahakama hizi za CCM kamwe haziwezi kutenda haki, zimewekwa MFUKONI na jiwe siku nyingi. Tuombe Mungu serikali hii ya WATEKA NYARA ifurumushwe kupitia uchaguzi Mkuu, iwe kwa kura ama MAANDAMANO YASIYO NA KIKOMO.
Wanaotenguliwa ni wa upinzani pekee CCM hatujawahi kusikia hata mmoja ametenguliwa. shame on them
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…