Wasio amini uwepo wa mungu Kenya wataka kuondolewa neno God kwenye wimbo wa taifa.

Wasio amini uwepo wa mungu Kenya wataka kuondolewa neno God kwenye wimbo wa taifa.

hazole1

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2015
Posts
4,319
Reaction score
3,916

Chama cha watu wasioamini uwepo wa Mungu (Atheists) nchini Kenya kimetaka kuondolewa kwa neno ‘God’ kwenye wimbo wa taifa.

Wanadai kuwa neno ‘God” kwenye mstari wa kwanza wa wimbo huo halihimizi moyo wa umoja kwakuwa si Wakenya wote wanaomuamini Mungu.

Wamedai kuwa Kenya ni nchi isiyo na dini na hivyo kuimba wimbo wa taifa wenye neno ‘God’ inakinzana na katiba ya nchi hiyo. Wimbo wa taifa wa Kenya huanza na kwa kusema “Oh, God of all creation.”

Watu hao wamesema kuwa huhisi kutengwa kila wimbo huo unapoimbwa. Wamesema watapeleka malalamiko yao bungeni.
 
Naona na akina Kiranga watasema neno Mungu ibariki litolewe ktk wimbo wa bongo
 
Wako sawa kabisa marekani yeye ile In God we trust katika dollar hio God hustand as In Gold Oil and Diamond we trust. Lakini kwa kenya na Tanzania hizi nyimbo humaanisha kweli mungu yule wa kufikirika ambae sie wa wote bali wa believers
 
Hao wapumbavu hawawezi kushinda ktk swala lao hilo la kipumbavu. Mungu Yupo na Alikwepo na Ataendelea kuwepo!

"Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameyaharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema" ZABURI 14:1
 
Wimbo wa Kenya first verse ni hii,
Eh Mungu nguvu yetu, ilete Baraka kwetu
Haki iwe ngao na mlinzi na tukae na undugu,amani na uhuru,raha tupate na ustawi
Hio 'God of all creation' mzee sijui umeipata wapi...
 
Back
Top Bottom