Chama cha watu wasioamini uwepo wa Mungu (Atheists) nchini Kenya kimetaka kuondolewa kwa neno ‘God’ kwenye wimbo wa taifa.
Wanadai kuwa neno ‘God” kwenye mstari wa kwanza wa wimbo huo halihimizi moyo wa umoja kwakuwa si Wakenya wote wanaomuamini Mungu.
Wamedai kuwa Kenya ni nchi isiyo na dini na hivyo kuimba wimbo wa taifa wenye neno ‘God’ inakinzana na katiba ya nchi hiyo. Wimbo wa taifa wa Kenya huanza na kwa kusema “Oh, God of all creation.”
Watu hao wamesema kuwa huhisi kutengwa kila wimbo huo unapoimbwa. Wamesema watapeleka malalamiko yao bungeni.
Wako sawa kabisa marekani yeye ile In God we trust katika dollar hio God hustand as In Gold Oil and Diamond we trust. Lakini kwa kenya na Tanzania hizi nyimbo humaanisha kweli mungu yule wa kufikirika ambae sie wa wote bali wa believers
Wimbo wa Kenya first verse ni hii,
Eh Mungu nguvu yetu, ilete Baraka kwetu
Haki iwe ngao na mlinzi na tukae na undugu,amani na uhuru,raha tupate na ustawi
Hio 'God of all creation' mzee sijui umeipata wapi...