Wasiokuwa tayari kuipigania katiba mpya waufyate

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Tuwe wawazi, tena kIroho safi tu.

Kupigania haki dhidi ya serikali za kiafrika si kazi ndogo:

Fu5j7XdXgAIMttn.jpeg

Mtanzania gani mwenye kuwa na uhalali (moral authority) wa kumbeza Odinga kwenye harakati za huko kwao?

Nisiwachoshe, tusichoshane.

"Katiba mpya tunayoitaka ya kupewa mezani haipo. Asiyekuwa tayari kuipigania na akae kimya tu."

Hao ndugu wanatupotezea muda bure.
 
Kelele za Katiba Mpya zimekwenda likizo, zimemezwa kwenye mdomo wa maridhiano.

Tusubiri Katiba Mpya tutakayoletewa na Ndumbaro.
Maccm walikipata cha moto enzi za Magufuli sidhani kama watafanya mzaha na katiba tena.
 
Cha moto walipata lakini kusubiria katiba mpya tunayoitaka ya kuletewa na wao, ni heri kusubiri kamba kupinda kwenye tundu la sindano.
 
Kupigania haki dhidi ya serikali za kiafrika si kazi ndogo:
Kupigania haki za Mwafrika dhidi ya Serikali....yeyote ile au zile zote za Ulaya na Marekani si Kazi ndogo. Waafrika wametokwa na Damu kupitiliza kiasi kudai haki zao....Kuanzia Mau Mau, Wakina Mkwawa na Kina Lumumba na Thomas Sankara na hata Martin Luther King na wengine. Ni upotoshaji wa hali ya juu kudai Waafrika ndio wabinya Haki wa dizaini ya Kukubuhu kuzidi Wazungu ambao mpaka hivi leo bado wana sheria zinazowabagua watu weusi na Wengine. Yaani kuna wengine walikuwa wameandika hata kwenye Katiba zao kuwa Mwafrika hana haki kabisa ya kudai haki.

Msitubeze
 
Wamesema mchakato wa Katiba mpya unaanza hivi karibuni lakini hakuna time frame utachukua muda gani.

Je kura ya maoni ya Katiba hiyo mpya itakuwa kabla ya Uchaguzi mkuu ujao?
 
Pa kuanzia ni kuwa na chaguzi huru, haki na kidemokrasia vyamani. Beberu kafanikiwa kwa sababu aliyaona haya mapema.

Viongozi wanapaswa kuchaguliwa na kuwapo madarakani iwapo tu wana majibu sahihi na yanayokubalika kuhusiana na agenda na malengo yetu.

Si pungufu wala zaidi. Yakikushinda hayo unafurushwa bila kukuangalia usoni kama yalivyo wakuta kina Liz Truss.
 
Kupigania haki za Mwafrika dhidi ya Serikali....yeyote ile au zile zote za Ulaya na Marekani si Kazi ndogo. Waafrika wametokwa na Damu kupitiliza kiasi kudai haki zao....Kuanzia Mau Mau, Wakina Mkwawa na Kina Lumumba na Thomas Sankara na hata Martin Luther King na wengine. Ni upotoshaji wa hali ya juu kudai Waafrika ndio wabinya Haki wa dizaini ya Kukubuhu kuzidi Wazungu ambao mpaka hivi leo bado wana sheria zinazowabagua watu weusi na Wengine. Yaani kuna wengine walikuwa wameandika hata kwenye Katiba zao kuwa Mwafrika hana haki kabisa ya kudai haki.

Msitubeze
Mkoloni mweusi anapojishasha kuwa yeye ana nafuu.

Mkuu mhuni ni mhuni tu!
 
Upo sawa Braza J Watanzania wanawajua wahuni.
Anathema is Anathema ask those who scripted your messages before you at the Exeter and Birmingham corridors of Shame.
 
Watanzania ndiyo sisi mjomba. Wahuni tunawajua. Wahuni ni wahuni tu. Wahuni hawawezi kubadilika!
 
Back
Top Bottom