Wasira afanya mazungumzo na spika wa Cuba

Wasira afanya mazungumzo na spika wa Cuba

Chifu mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2025
Posts
422
Reaction score
489
By Maulid Mmbaga , Nipashe


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Baraza la Taifa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Cuba Esteban Lazo Hernandez na ujumbe wake.

Kwa mujibu wa taarifa ya CCM Wasira amefanya mazungumzo na ujumbe huo uliofika kwenye ofisi ndogo ya CCM Lumumba, Dar es Salaam leo Machi 6, 2025.

Katika mazungumzo na ujumbe huo kutoka Cuba wameahidi kuendeleza ushirikiano wa kihistoria kati CCM na Chama cha Kikomunisti cha Cuba, pamoja na Tanzania na Cuba.
 
Cuba Esteban Lazo Hernandez na ujumbe wake.

06 March 2025

President of the Cuban Parliament begins official visit to Tanzania​

Before leaving for Tanzania, Lazo Hernández visited the headquarters of Zimbabwe’s National Assembly

f0039123.jpg

Esteban Lazo Hernández held an emotional and fruitful exchange with Cuban collaborators in the sister nation. Photo: Enrique Moreno Gimeranez

Dar Es Salaam, Tanzania. -The member of the Political Bureau of the Party and president of the National Assembly of People's Power, Esteban Lazo Hernández, arrived yesterday in the United Republic of Tanzania, on an official visit.

On the same day, he held an emotional and fruitful exchange with Cuban collaborators in the sister nation, with whom he shared on national current affairs, the work of the Cuban Parliament, and the history of bilateral friendship, among other aspects.

IN THE PARLIAMENT OF ZIMBABWE
Before leaving for Tanzania, Lazo Hernández visited the headquarters of Zimbabwe’s National Assembly, where he was received by his counterpart, Jacob Mudenda, with whom he held official talks.

He highlighted the historic ties of friendship and cooperation, and the willingness to continue working for their strengthening and expansion.
"Our visit is part of the celebration of the 45th anniversary of the establishment of diplomatic relations between both nations," said Lazo.

He urged both Parliaments to consolidate actions and initiatives in view of the commemoration of these years of ties and solidarity cooperation, forged on the basis of the legacy of the close friendship between Robert Mugabe and Commander-in-Chief Fidel Castro Ruz
Source : Granma
 

Rais wa Bunge la Cuba afanya mazungumzo na viongozi wa juu wa Zanzibar​

Uhusiano kati ya Cuba na Tanzania unatokana na urafiki wa karibu kati ya Fidel Castro na Julius Nyerere

Machi 6, 2025 10:03:31
f0039131.jpg

Picha: Enrique Moreno Gimeranez
Zanzibar, Tanzania.— Akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama, Esteban Lazo Hernandez aliye pia Rais wa Bunge alifanya mazungumzo rasmi na Dr. Hussein Ali Mwinyi, rais wa Zanzibar, katika Ikulu ya Zanzibar.

View: https://m.youtube.com/watch?v=TBZESSA_XVw
Katika mazungumzo hayo ya kindugu, Lazo Hernández alisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Cuba na Tanzania, kwa kuzingatia urithi wa urafiki wa karibu kati ya Fidel Castro na Julius Nyerere.


Alitoa shukrani zake kwa uungwaji mkono wa Tanzania kushindikiza kusitishwa vikwazo dhidi ya Cuba na wito wa Tanzania kutaka kuondolewa Cuba kutoka orodha ya wafadhili wa serikali za kigaidi.

Rais Dr. Hussein Ali Mwinyi alieleza kushukuru sana kwa mshikamano wa jadi, uungaji mkono wa Cuba kwa Zanzibar na mchango wa Cuba katika kupata uhuru wa nchi kadhaa za Afrika. Alituma salamu zake kwa Katibu wa Kwanza wa Kamati Kuu ya Chama na Rais wa Jamhuri, Miguel Díaz-Canel Bermúdez.

Baadaye, Lazo Hernández alikuwa na mazungumzo na Zubeir Ali Maulid, spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Pande zote mbili zilikubaliana juu ya nia ya mabunge hayo mawili kuunga mkono uimarishaji wa mahusiano ya ushirikiano.

Rais wa Bunge la Cuba pia alitembelea maeneo ya Kiwanda cha Kuangamiza Malaria kilichopo Kibaha, mkoa wa Pwani chenye msaada wa kitaalamu kutoka Kampuni kubwa ya Antilles kutokana na nia ya Serikali ya Tanzania katika kupambana na ugonjwa wa Malaria katika Tanzania.

Source : Granma
 
Back
Top Bottom