Wasira: CCM kujifanyia tathmini unalenga kuboresha uongozi na kutatua changamoto za wananchi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kuagiza chama kujifanyia tathmini unalenga kuboresha uongozi na kuhakikisha changamoto za wananchi zinashughulikiwa ipasavyo.

Wasira amesema katika kuelekea uchaguzi mkuu wa CCM, ni muhimu kwa wanachama na viongozi kujipima kabla ya kuomba nafasi za uongozi ili kuhakikisha wanakidhi vigezo, ikiwemo uadilifu na uwezo wa kiutendaji.

Amesema hayo jana, Mei 15, 2026, mkoani Kigoma alipokutana na viongozi wa CCM katika wilaya za Buhigwe na Kasulu pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa, akiwa katika ziara ya kichama.

Soma Pia: Wasira: CCM Haibebwi, inafanikiwa kwa ukubwa wake na Imani ya Wananchi

Katika maelezo yake, Wasira amesisitiza umuhimu wa kuzingatia Katiba, kanuni na miongozo ya CCM, akibainisha kuwa uongozi bora unapatikana kwa kufuata misingi iliyowekwa na chama.

Your browser is not able to display this video.
 
CCM mlishajifia kifo cha mende. Acheni kupoteza raslimali muda na fedha kwenye jambo lisilo tekelezeka. Nyinyi ni wezi wa kura mliokubuhu! Ni mwananchi gani mwenye akili timamu atawaamini?
 
CCM.kwa sasa imekuwa mkono wa shetani wa kuwaletea mateso na vifo watanzania.

Kuiunga mkono CCM.ni kuunga mkono mauaji ya binadamu wrnzako.

CCM haifai hata kuwa chama cha upinzani, inatakiwa wananchi waifute moja kwa moja, ibakie tu kwenye historia kwamba kulwahi kuwa na chama cha hovyo kilichowabi kuua maelfu ya Watanzania ili kupora madaraka.

Ewe Mtanzania mwenye kuipenda nchi yako jitenge na shetani CCM, baba wa uovu wa kila namna.

Kwa mtu yeyote mwadilifu mwenye Roho wa Mungu, hakuna tusi baya kama kuitwa mwanaCCM!
 
The Muzee is very brilliant politically speaking
 
 
Ila CCM wana dhambi sana wamemchukua huyu kiumbe toka hifadhi ya Gombe ili awe kivutio kwenye mikutano yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…