Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakuu
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira, akizungumza katika Kongamano la Wanawake lililofanyika jijini Dodoma leo, Februari 4 amedai "Siku hizi wako watu nje ya Tanzania, na wana Vibaraka ndani ya Tanzania ambao wanasema CCM mmekaa sana madarakani. Na mimi nawauliza tulipodai uhuru kwanza mlikuwa wapi? na nani ambaye ulisaini naye mkataba kwamba tukijitawala tutakuwepo kwa muda fulani, nani aliwaambia?"
"Sisi tunaongoza dola kwa idhini ya Watanzania na Watanzania wakituendelea kutuamini tutaendelea kuongoza dola na mtu yeyote asituulize kwanini tunaendelea kuwepo, wanasema mambo ya ajabu na wengine ni vibaraka wakubwa wakwenda kutuletea utamaduni usioeleweka wanasema Wanawake waoane kwa Wanawake na Wanaume waoane kwa Wanaume, hayo mambo ya Ushoga wapi na Mungu aliumba watu tofauti kwa kazi tofauti"
"Ndio maana Rais Museveni aliwaambia wakubwa wa Ushoga, kwamba akikuta mashoga atawafungia jela na atawatoa endapo mwanaume mmoja atapata mimba..."
Soma, Pia: Wasira: Mabeberu na Vibaraka wao wanataka kuleta Ushoga