Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa mgawanyiko ndani ya CHADEMA unazidi kudhoofisha nafasi ya chama hicho kushindana na CCM katika uchaguzi ujao, akisisitiza kuwa hadi sasa hakuna chama mbadala chenye uwezo wa kuiondoa CCM madarakani.
Akizungumza na wananchi wa Bariadi, mkoani Simiyu, siku ya Jumatatu Februari 10, 2025 Wasira amesema kwamba migogoro inayokumba upinzani, hususan CHADEMA, imewaacha wakiwa dhaifu na kwamba nafasi yao ya kuingia Ikulu ni ndoto isiyowezekana.
"Tumemaliza kazi, tunawasubiri watani zetu wa jadi. Kwa hali ilivyo na kwa ugomvi uliopo kwenye chama chao, Ikulu wataiona kwenye runinga," amesema Wasira.
Soma: Wasira: CHADEMA Urais mtauona kwenye Runinga pekee
Ameendelea kueleza kuwa mvutano ndani ya chama hicho umeathiri mshikamano wao, akitolea mfano kile alichodai kuwa mgawanyiko uliotokea jijini Dar es Salaam baada ya Mkutano Mkuu wa CHADEMA wa kumpata mwenyekiti wake.
"Hawa waliokuwa wanatukanana pale Dar es Salaam mpaka wamegawana fito- mtu mmoja amekimbia na fito zake, mwingine amebaki na zake. Pale hakuna CHADEMA, kuna nusu CHADEMA. Nusu imekimbia, nusu imebaki," ameongeza.
Wasira amesisitiza kuwa CCM kama chama kikubwa barani Afrika, hakiwezi kushindana na chama kilichogawanyika.
"Sisi kama chama kikubwa kuliko vyote Afrika, tunaweza kushindana na nusu CHADEMA? Tumewaambia waje basi, na sisi tupo tayari, na ushindi ni lazima," amesema kwa msisitizo.