Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Unaweza ukawa ni mvutano mpya kuhusu Katiba kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Stephen Wasira, kusema kuwa hoja ya kutaka mabadiliko ya Katiba kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 imechelewa.
Wasira ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Januari 23, 2025 jijini Dodoma katika hafla ya mapokezi katika makao makuu ya chama hicho, ikilenga matamshi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, ambaye alisema, "hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi."
Pia, Soma: Naibu Katibu Mkuu CHADEMA: Bila mabadiliko, 2025 hakutafanyika Uchaguzi wowote
Akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Lissu alisisitiza kuwa mabadiliko ya Katiba ni lazima kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Mvutano huu unaonyesha changamoto zinazozikumba juhudi za kutafuta maridhiano ya kitaifa, huku uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ukikaribia.
Lissu, alisema Chadema inakubaliana na wazo la maridhiano, lakini kwa sharti kuwa yatakuwa na mwelekeo chanya.
Alisema: "Kama hakuna Katiba mpya, basi hakuna uchaguzi."