Lazima hao viumbe wa majini wajipatie kitoweo hapo!
Stupid Kima!Akizungumza Julai 20, 2026 kwenye kipindi cha Dakika 45 cha ITV, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesisitiza kuwa hakuna Katiba ya Jaji Warioba bali Tume hiyo iliundwa kwa aajili ya kukusanya maoni tu.
"Tume ya Jaji Warioba ilikuwa haiandiki katiba. Ilikuwa na kazi moja tu; kukusanya maoni na kuwasilisha katika Bunge la Katiba. Ilifanya kazi yao nzuri tu. Wala hatuna madai nayo. Lakin kuna watu wanasema wanataka katiba ya Warioba. Warioba hana katiba. Warioba hana katiba, haitowi Warioba, na katiba haiwezi kuwa ya mtu. Katiba ni ya watu. Na sheria hii iliyompa Warioba kukusanya maoni ndiyo sheria iliyosema ipelekwe Bunge, na Bunge lilifanya kazi yake. Wao ndio waliokimbia wapinzani hao".
Ukisikia kuzeeka siyo mawili tu bali pia na akili.Akizungumza Julai 20, 2026 kwenye kipindi cha Dakika 45 cha ITV, Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesisitiza kuwa hakuna Katiba ya Jaji Warioba bali Tume hiyo iliundwa kwa aajili ya kukusanya maoni tu.
"Tume ya Jaji Warioba ilikuwa haiandiki katiba. Ilikuwa na kazi moja tu; kukusanya maoni na kuwasilisha katika Bunge la Katiba. Ilifanya kazi yao nzuri tu. Wala hatuna madai nayo. Lakin kuna watu wanasema wanataka katiba ya Warioba. Warioba hana katiba. Warioba hana katiba, haitowi Warioba, na katiba haiwezi kuwa ya mtu. Katiba ni ya watu. Na sheria hii iliyompa Warioba kukusanya maoni ndiyo sheria iliyosema ipelekwe Bunge, na Bunge lilifanya kazi yake. Wao ndio waliokimbia wapinzani hao".
Hapo hawatoboi wallah😀
Ufafanuzi dhaifu sana huu kutoka kwa mtu mwenye hadhi yake!
Unadhani hajui, ni kujitoa tu UFAHAMU!Ufafanuzi dhaifu sana huu kutoka kwa mtu mwenye hadhi yake!
Kusema 'katiba ya warioba' ni kurahisisha mrundikano wa maneno yanayo maanisha 'Rasimu ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya iliyosimamiwa na Warioba'.
Hivi kuna mtu mwenye akili timamu akisema ... 'ya warioba'... Anakuwa kamaanisha kuwa ni mali ya Warioba ile realy!
Mbona hawa watu hawataki kushusha presha zetu?
Hakuna hotuba ya viongozi sasa hivi inayoweza kutolewa ikawafurahisha wananchi.
Ni majigambo na ubabe kwa kwenda mbele, sijui nani kairoga Serikali ya awamu hii!