Elections 2010 Wasira: Msiuze urais kwa 20,000/-

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Wasira: Msiuze urais kwa 20,000/-
Imeandikwa na Mgaya Kingoba, Bunda; Tarehe: 25th September 2010 @ 23:40 Imesomwa na watu: 152; Jumla ya maoni: 0



Habari Zaidi: Kituo cha polisi Dar es Salaam chakumbwa na kashfa
Wasira: Msiuze urais kwa 20,000/-
Meza ya urithi Dar es Salaam yazua mtafaruku
Kikwete aonesha ufugaji wa kisasa
CCM Iringa wahaha kunusuru jimbo
Vigogo Newala kortini kwa rushwa
JK: Mpeni kura Jah People, atawasaidia
CCM walia rafu za kampeni Vunjo, Moshi Vijijini
Wakulima wa chai Lupembe wapewa faraja
Polisi yamtaka mgombea Chadema afuate ratiba
Tanzania, Kenya zatoa mil. 750/- kuangamiza viwavi jeshi
Viongozi wa wafanyakazi watakiwa kuwa mfano
Mtoto `atekwa’ shuleni kwake Dar es Salaam na kutoroshwa
JK:Hifadhi hazitaathirika
Chipaka apinga Wakenya kufundisha Watanzania Katiba
Mwanafunzi afa maji bwawani
Polisi apigwa mapanga, `Defender’ lavunjwa kioo
Wenye VVU wafundwa kuepuka unyanyapaa
Asasi za kiraia zaungana kufuatilia uchaguzi mkuu
Waislamu kuelimishwa kuhusu Hijja

Habari zinazosomwa zaidi: Balaa lingine kwa Chenge
Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
Vatican yamvua jimbo Askofu
Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
MG O M B E A ubunge kwa tiketi ya CCM katika Jimbo la Bunda, Steven Wasira amewataka Watanzania wasifanye majaribio na kubahatisha katika kuchagua urais kwa sababu mamlaka hayo ni makubwa na yanastahili kukabidhiwa kwa mtu mwenye akili timamu na chama cha maana.

Aidha, amehoji kwa vipi Watanzania wanaweza kununua urais kwa Sh 20,000, akihusisha na kauli ya mgombea urais wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa aliyekaririwa akisema akishinda, atafuta ada katika shule nchini.

Kwa sasa, ada kwa shule za sekondari za kutwa za serikali ni Sh 20,000 wakati elimu ya msingi hakuna ada. Kwa elimu ya chuo kikuu, serikali inatoa mikopo.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni mjini Bunda mbele ya mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, Wasira alisema urais ni mamlaka makubwa ambayo Watanzania hawapaswi kuyafanyia majaribio.

“Mwisho nataka kutoa ushauri kwa watu wa Bunda, Mkoa wa Mara na kwa Watanzania wote. Kwa mujibu wa Katiba yetu, mamlaka ya kiongozi wa serikali huchaguliwa na wananchi.

Rais ni mamlaka makubwa,” alisema. “Ndiye anayetangaza vita, kwa hiyo usiende kubahatisha, wala msifanye mambo ya kubahatisha, kujaribu.

Ni lazima mchague mtu mwenye akili timamu, anayetoka chama cha maana. Mwalimu Nyerere alisema Rais anaweza kutoka chama chochote, lakini Rais bora atatoka CCM.”

Huku akishangiliwa na wananchi, mwanasiasa huyo ambaye pia ni maarufu kwa jina la Tyson, alisema Watanzania ifikapo Oktoba 31, mwaka huu, hawapaswi kuchagua Rais wa kubahatisha, wa kudanganya na msema uongo.

“Mtu anasema atauza saruji kwa shilingi elfu tano…kiwanda anacho?

Bei ya mafuta inapangwa duniani na ina uhusiano na mataifa mengine katika masuala ya uchumi, yeye atamudu vipi,” alihoji Wasira ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.
 
Hiyo alfu ishirini hatujapokea kwa mtu wala siyo kwamba kwa sababu ya elimu tu ndo tumchague slaa. bali kwa umakini, uzalendo na nia ya kurejesha heshima ya serikali.

au wassira anatuasa tuuze urais wetu kwa kofia na tisheti?

Wassira anajilinganishaje yeye na halmashauri yake na ile ya karatu? anaingia kwenye viatu vile????
KARATU boy ndiye tunayempigia chapuo awe raisi ili yale aliyoyaweza kule jimboni kwake yawezekane nchi nzima.
 
Wasira nae sasa chama chake kinacho nunua kura kwa elfu 2,5, 10 na khanga na t-shirt juu sijui haoni?
 
Basi tutauza urais kwa Tshirt na khanga !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…