Pre GE2025 Wasira: Uchaguzi wa CHADEMA, viongozi wa kitaifa waligawana fito

Pre GE2025 Wasira: Uchaguzi wa CHADEMA, viongozi wa kitaifa waligawana fito

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira amesema chama hicho kimedhamiria kuleta mapinduzi katika maisha ya wananchi huku akitumia vijembe kwa Chadema kuwa katika uchaguzi wa viongozi wa kitaifa waligawana fito.

Soma Pia: Wasira: Watanzania hawana sababu ya kuichagua CHADEMA

Wasira amesema hayo leo Jumamosi, Februari 8, 2025 alipokuwa akizungumza na Wana-CCM alipowasili kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara na kueleza kuwa CCM itaendelea kuwatoa Watanzania katika hali duni na kuwajengea misingi ya maisha bora kadiri inavyowezekana.

 
Hizo fito zikowapi?Ujinga mtupu,mpaka matundu ya vyoo kwa hisani ya Wamarekani
 
Fito kwamba lissu + Lema walitumia matusi dhidi ya Mbowe
Akili za wanaccm ni upumbavu mtupu. Ndio maana nchi ina miaka zaidi ya 60 lakini wanaiita changa.
Hata madawati tu yakutosheleza watoto wetu wameshindwa
 
Wakati huo huo, ule mkutano wa CCM kule Dodoma iliishia kwa wanaCCM wakigawana jembe na nyundo, huku wakitoka na manung'uniko wakisema safari hii hakuna tena kulima wala kujenga ni mwendo wa kuuana, kuchimba makaburi na kuzikana.
Tunasubiri muda useme kitu.
 
Aliyepigwa au kutukanwa kama mnavyodai basi alideserve shida iko wapi?

Mmempa babu aitaje chadema 3x per day kama dose ya malaria? Anaacha kueneza sera za chama
 
Back
Top Bottom