Wasiwasi juu ya madokta wa Tz kwenda kanda zenye Ebola

Maserati

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2014
Posts
11,604
Reaction score
20,085
Habari wana Jf, hivi jamani hawa madaktari wa Hapa nchini Tz kwenda kujitolea huko kwenye kanda zilizo athiriwa na ugonjwa wa Ebola haitaleta tafrani hapa kwetu? Maana hata madaktari wa kimarekani na wengine walioenda huko wachache miongoni mwao wamepatikana na virusi vya Ebola na kurudishwa nchini kwao na miongoni mwao wamefariki japokuwa nchini kwao wana dawa na kinga pia wanasema zipo kwenye majaribio. Je, hawa wa kwetu wameenda huko ilhari Tz hatuna hata mzizi mmoja ambao unasemekana utawatibu, watambulia panadol tu. Wakirudi hapa si ndio mwanzo wa tafrani, watapewa dawa gani hapa? Si ndio mwanzo wa kusambaa kwa ugonjwa huo nchini kwetu jamani. Mambo mengine tunajitakiwa. Wengi wetu masikini sisi, tamaa zao za pesa zitatumaliza nchi nzima..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…