ndugu wana JF hatua tuliofikia sasa hivi kwenye mchakato wa katiba mpya ni kukutana kwa mabaraza ya katiba na kutoa maoni waliopendekezwa na wananchi kuhusu rasimu ya katiba mpya iliyotolewa na tume ya warioba...mabaraza ya katiba ni kwaaajili ya kufikisha maoni yaliotolewa na wananchi kuhusiana na rasimu ya katiba mpya iliotolewa na tume ya mabadiliko ya katiba..kitu kilichonishtua nimerudi likizo nipo kijijini rasimu za katiba zimetolewa na serikali na katika kijiji chetu zimetolewa rasimu 40 ambazo wananchi wanatakiwa waende waketi hapo apo kijijini wasome alafu watoe maoni wao...hili naona litanyima fursa kwa wananchi kuweza kupata kujua haswa kwa nini kilichoandikwa kwenye hiyo rasimu.kama tunavojua kuwa katiba ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa na sisi kama watawaliwa tunatransfer power kwa viongozi lakini haimaanishi sisi tunapoteza power na katiba yoyote ili iwe na legitimacy acceptance of the people lazima itokane na watu wenyewe..wasiwasi wangu mwingine ni juu ya CCM kuonekana kudominate process nzima ya katiba kwa maslahi yao binafsi na si kwa maslahi ya wananchi..kuna watu wengi hapa kijijini hawajui nini maana ya katiba na katiba itawasaidiaje wao kama wao..utaingiaje mkataba huku hujui mkataba wenyewe unakusaidiaje...serikali imekimbilia kwenye swala la katiba bila ya kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi wao na kuna dalili ya kupata katiba mbaya kuliko ambayo tulokua nayo kwani rasimu ni only one step of the process na wasilisha