Waso na maono,watawachagua.

Waso na maono,watawachagua.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
WASO NA MAONO,WATAWACHAGUA

Naam
Haina ubishi,hao
Wasojitambua
Wasojielewa
Waso na maono.

Tuseme tu
Ndio wao,viherere
Barabarani,na vikengele
Vigelele,wapiga makofi
Tutawachagua.

Tena
Kwa mara nyingine
Tuwape ulaji
Wale,wanenepe
Si ndio.

Hivyo
Tena,hivyo hivyo
Ndivyo tunataka,tumelogwa
Tena mchawi,amekufa
Labda kwa ngoma,ama Corona
Tuna balaa.

Watachagua
Waso na akili
Hawana malengo,limradi
Siku ziende
Mahohehahe

Wasobadilika
Kila siku wale wale
Wanaogopa
Wakijitisha
Watetemeka.


Watawachagua
Ili tuteseke,tutaabike
Sisi na wao,wao si sisi
Waso na maono,ndio mikosi
Tufanye nini.


Tuamueni
Tuwatoeni,tuwatimue
Watukimbie,walikotoka
Tumewachoka ?
Hatuwataki.

Kweli
Waso na maono
Watawachagua
Watowachagua
Hawana maono.

Idd Ninga
Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom