Sio mara moja au mbili bali ni mara kadhaa ninapo sikiliza taarifa au kuangalia runinga kwa ajili ya kupata habari huwa ninawasikia watangazaji wanatamka kwa mfano ...katika ajali hiyo abiria X wameweza kupoteza maisha yao... au katika shambulio hilo ....wanawake na watoto waliweza kupoteza maisha ya ... labda uelewa wangu ni mdogo kwani hao wanaosmekana kuweza kupoteza maisha yao walipanga kuyapoteza? au kwa maana nyingine hao waliopoteza maisha walikuwa na mawasiliano na ajali au wafanya mashabulizi??i ina maana kwa kufikia vifo vyao ni mafanikio kwao? PLEASE HELP TUBORESHE HABARI