Wasomaji wa utabiri wa hali ya hewa wabadilike!

Wasomaji wa utabiri wa hali ya hewa wabadilike!

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,203
Reaction score
37,906
Moja kwa Moja kwenye mada!

Ukiskiliza Tabiri za Hali ya Hewa kwenye Vyombo vingi vya Habari ni kawaida kuskia sentensi kama hizi "......Maeneo ya Pwani..... Maeneo ya kati ya Nchi pamoja na Kusini kwa Mkoa wa Morogoro.... kutakuwa na Mvua za Hapa na Pale..... kutakuwa na Mvua Kiasi.... na vipindi vifupi vya Jua...." Aina hii ya Uchaguaji wa Maneno ama Maelezo ya aiona hii haimsaidii Mwananchi wa Kawaida....

Mkulima, Mmachinga, Mfugaji kudadavua specifically nini kimelengwa hapo! Ni kama Maelezo hayo wanayatoa kwa ajili yao wenyewe watumishi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa. Hizi ni Jiografia za darasa la 4 huko lkn sio wote walisoma na si wote wanakumbuka kwamba NJOMBE na IRINGA ni Nyanda za Juu kusini!

Sio wananchi wengi wanaelewa inapotajwa KUSINI KWA MKOA WA MOROGORO.... Vipindi vifupi vya Jua..... Mvua za Hapa na pale... athari zake ni pamoja na Wananchi kushindwa kufanya maamuzi juu ya kile walichokiskia. Sijui kwa nini hawawezi kusema mf tu.... mikoa ifuatayo kesho itapata Mvua... Tanga, DSM, Pwani na Kagera.... nk...

Nadhani wanahitaji kubadilika kwa Maslahi wa Wanannchi wote.
 
Wewe ndio wa kubadilika kwa kuacha kuwaangalia. Hao watabiri wa hali ya hewa huwa ni waongo wakubwa, siku zote tabiri zao husukumwa na uhalisia wa hali ya hewa wa siku husika. Wakiona leo imenyesha mvua basi utasikia na wao wanaunganisha kuwa siku ifuatayo kutakuwa na mvua.

Mara nyingi huingiza watu mkenge kwa tabiri za uongo.
 
Jamaa huwa wanatumia njia ya analogy mkuu. Wanafanya prediction tu. Mfano; wanaangalia katika siku/tarehe Kama hiyo kwa miaka labda 5 au 10 nyuma kulikuwa na hali gani? Then probability kubwa ndio wanaiweka.
Hatuna radar za kisasa za kusoma miezi/siku kadhaa mbele Kama wafanyavyo walioendelea kisayansi.
 
Back
Top Bottom