Wasomali wapewa ekari 100 kinyemela Rufiji

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
Rufiji: Watu wawili wanaodaiwa kuwa raia wenye asili ya Somalia, wamepewa ekari 100 za ardhi na Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Kata ya Chumbi, wilayani hapa bila kushirikisha wananchi wala uongozi wa wilaya.

Wakizungumza wilayani hapa juzi, baadhi ya wananchi walisema raia hao mmoja hawezi kabisa kuzungumza Kiswahili, walikabidhiwa eneo hilo karibu na ilipokuwa Shule ya Msingi Chumbi C.

Inadaiwa Wasomali hao wameweka kambi eneo la shule, wamekwenda Dar es Salaam kwa mapumziko ya Sikukuu ya Pasaka na wanatarajia kurejea wiki ijayo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Athuman Mtimbuko alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, alisema hayupo tayari kuzungumza na mwandishi wa habari hizi kwa sababu ana ugomvi binafsi.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Chumbi, Bakari Ngongota alipoulizwa kuhusiana na Wasomali hao, alisema amepata taarifa zao na waliofika kijijini hapo kuomba ardhi kwa ajili ya kilimo cha mtama, walipewa na halmashauri ya kijiji.

Ngongota alisema uongozi wa kijiji hicho umekuwa ukitoa ardhi ovyo bila kumpa taarifa na kwamba, mambo ya kijiji hicho yamekuwa yakifanyika kwa siri na kuahidi kufuatilia zaidi.

Ngongota alisema ameelezwa na ofisa mtendaji wa kijiji kuwa, watafanya mkutano wa kuwatambulisha Wasomali hao wiki ijayo lakini hawakutoa taarifa rasmi kwake hadi alipouliza.
 
Duh...hatimaye tutakuwa wakimbizi ndani ya nchi yetu
 
Wamejaa sana kwenye nchi yetu wanaingia kwa style ya kulima tena wanaanzisha miji yao kwenye mapori baada miaka michache wanaingia kwenye active politics au business
 
Wapi wameanzisha mji wao huu sii uongo pia angekua mwekezaji mzungu au muatabu mngefurahia lakini black investers inakua nongwa
Utumwa unatusukuma kua muafrica hawezi kuwekeza
Acheni chuki. Wao ni wawekezaji kama wengine
 
ardhi.jpg

KWA UFUPI
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Athuman Mtimbuko alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, alisema hayupo tayari kuzungumza na mwandishi wa habari hizi kwa sababu ana ugomvi binafsi.

Rufiji: Watu wawili wanaodaiwa kuwa raia wenye asili ya Somalia, wamepewa ekari 100 za ardhi na Halmashauri ya Kijiji cha Chumbi C, Kata ya Chumbi, wilayani hapa bila kushirikisha wananchi wala uongozi wa wilaya.

Wakizungumza wilayani hapa juzi, baadhi ya wananchi walisema raia hao mmoja hawezi kabisa kuzungumza Kiswahili, walikabidhiwa eneo hilo karibu na ilipokuwa Shule ya Msingi Chumbi C.

Inadaiwa Wasomali hao wameweka kambi eneo la shule, wamekwenda Dar es Salaam kwa mapumziko ya Sikukuu ya Pasaka na wanatarajia kurejea wiki ijayo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Athuman Mtimbuko alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, alisema hayupo tayari kuzungumza na mwandishi wa habari hizi kwa sababu ana ugomvi binafsi.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Chumbi, Bakari Ngongota alipoulizwa kuhusiana na Wasomali hao, alisema amepata taarifa zao na waliofika kijijini hapo kuomba ardhi kwa ajili ya kilimo cha mtama, walipewa na halmashauri ya kijiji.

Ngongota alisema uongozi wa kijiji hicho umekuwa ukitoa ardhi ovyo bila kumpa taarifa na kwamba, mambo ya kijiji hicho yamekuwa yakifanyika kwa siri na kuahidi kufuatilia zaidi.
Ngongota alisema ameelezwa na ofisa mtendaji wa kijiji kuwa, watafanya mkutano wa kuwatambulisha Wasomali hao wiki ijayo lakini hawakutoa taarifa rasmi kwake hadi alipouliza.
Wasomali wapewa ekari 100 kinyemela Rufiji - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Back
Top Bottom