Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Wasomi Mlimani kizimbani kwa wizi NMB
Yaelezwa walitumia simu za mkononi kuibia wateja
na Julieth Mkireri, Kibaha
UMEIBUKA mtindo mpya wa wizi wa fedha katika Benki ya NMB kwa kutumia teknolojia ya simu za mkononi, ambapo wanafunzi watano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Pwani kwa tuhuma za wizi wa sh 20,280,000 unaodaiwa kufanywa kwa njia hiyo.
Wizi huo unadaiwa kufanywa na wanafunzi hao Desemba mwaka jana kwa mbinu mpya ya kutumia simu zao za mikononi katika kuiba fedha za wateja wa benki hiyo ya wananchi ambayo inatumiwa na wafanyakazi wengi wa serikali.
Wanafunzi hao ambao walifikishwa mahakamani jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mkoa, Nsekela Mwaiseje, kujibu tuhuma hizo wametajwa kuwa ni Boniface Kyaga (23) anayedaiwa kuiba sh 9,030,000 na David Mwani sh 4,900,000.
Wengine ni Deodatus Buyokwe anayedaiwa kuiba kiasi cha sh milioni tano, Idota Makena, anayedaiwa kushiriki zoezi hilo na kujipatia sh laki tisa na Gloria Joseph anayetuhumiwa kuiba sh 450,000 kwa kutumia njia hiyo hiyo ya simu ya mkononi.
Akielezea kuhusu tukio hilo la wizi, Mwendesha Mashitaka, Mrakibu wa Polisi Hatib, aliweka bayana mbele ya Hakimu Mwaiseje kuwa wanafunzi hao wa Chuo Kikuu Mlimani waliiba fedha hizo zote zikiwa za wateja wawili wa benki hiyo ya NMB Tawi la Rufiji, mkoani Pwani.
Washitakiwa wote watano walikana mashitaka hayo na kesi yao imetajwa kusikilizwa tena Februari 8, mwaka huu.
Idota Makena na Gloria Joseph waliachiliwa baada ya kudhaminiwa na wakazi wawili wa Kibaha kwa dhamana ya sh milioni moja kila mmoja, wakati wanafunzi wengine watatu waliobaki walishindwa kutimiza masharti ya dhamana, hivyo kuendelea kubaki rumande.
Polisi inaendelea na uchunguzi kuhusu madai ya wateja wengine 20 wa benki hiyo Tawi la Kibaha, wanaodaiwa kuibiwa kwa njia hiyo, akiwamo mwandishi wa Radio One Mkoa wa Pwani, Ayoub Mtawazo.