Habari zenu wana JF, Ni mwezi mmoja sasa umepita binti mmoja jirani yangu amegoma kuolewa na mwanaume ambaye ni Dereva na kutoa maelezo yafuatayo.
- .Hataki mwanaume Dereva
- Askari aina zote
Eti anadai kuwa aina hizo za wanaume huwa wanatoka sana nje ya ndoa. Alichoniacha hoi ni pale alipodai kuwa Wasomi wa IT ndio wanaoongoza kwa utulivu kwenye ndoa. Nilipomuuliza sababu hakunieleza hivi hili nalo ni kweli kuwa wasomi wa IT ndiyo watulivu zaidi? kama ni kweli ni kwanini? Na kuna ukweli kuwa
baadhi ya fani zinaongoza kwa kuwa na mafataki?