Wasomi wa Tanzania Bado hatujalisaidia Taifa vya Kutosha

Wasomi wa Tanzania Bado hatujalisaidia Taifa vya Kutosha

yugoslav

Member
Joined
Mar 17, 2017
Posts
93
Reaction score
72
Nimekaa na kufikiri namna ambavyo wasomi wa Taifa hili tulivyolisaidia Taifa letu. Nimekuja kugundua na kuhitimisha kuwa elimu tunayopata darasani, iwe katika nchi za wenzetu au masomo ndani ya nchi, hayanufaishi Taifa (Nitaelezea mda nikipata)

Katika safari yangu ya masomo ya miaka 27 (ukiondoa elimu ya Musingi na Sekondari) katika nchi, za Scandinavia, Pacific na Urusi ya zamani kwa kazi ninayofanya haijafikia hata 1/8 ya elimu niliyonayo kichwani mwangu. Ni kweli tunaona dhamira chanya ya Mh. Rais ya kulipeleka Taifa katika uchumi wa kati.

Hata hivyo, je ni kwa kiasi gani Serikali inawawezesha wasomi wa nchi hii kuipeleka nchi katika huko tunakokutaka (uchumi wa viwanda)? Aslani ni kwa kiasi kidogo sana.

Kwa nini wasomi tutumie rasilimali nyingi [ikiwemo muda wa miaka mingi kusoma masomo magumu nje ya nchi na hata ndani ya mipaka ya nchi] na baada ya hapo ukirudi nchi hainufaiki na tulivyovisoma nchi za wenzetu!!!! Ni hatari sana.

Kuna rafiki yangu Mturuki nilikuwa nikisoma naye Scandinavian Academy of Aeronautics [Gothenburg], nitatumia jina la Kaplan] siyo jina lake halisi. Kaplan alikuwa akisoma 'combustion engineering technologies' na mimi nikisoma Aeronautical Engineering aliwahi kinieleza kuwa kutokana na elimu yake aliyoitafuta kwa muda wa miaka minane katika eneo hilo la 'combustion engineering technologies' nchi yake itanufaika vilivyo kwa kodi atakayoilipa kutokana kiwanda chake cha injini atakachokianzisha baada ya kuhitimu masomo yake.

Nilistaajabu kwa kauli hiyo kwa kuwa jamaa nilikuwa nikimjua maisha yake kwa muda wa miaka mitatu mfululuzo na hatakuweza kutabiri maisha ya wazazi wake kule nyumbani kwao kuwa hayatofautiani sana na maisha ya wazazi wangu nyumbani kwetu Tanzania.

Ndiyo, nilikuwa sawa kwa kadiri ya naelezo ya bwana Kaplan nikifananisha ya maisha ya nyumbani kwetu Tanzania. ........ Miaka minane baada ya kumaliza masomo yake ndoto ya Kaplan ilikuwa imetimia huku akiwa na harakati za kujenga viwanda vingine katika nchi za jirani.

Je mimi katika safari yangu ya miaka 27 niko wapi? Je kwa nini niko hapa?
***** Nitaendelea kuwaelezea.
 
Na wewe nenda Wizara inayohusika na hicho ulichosomea ili wakuwezeshe kulisaidia taifa lako.
 
Mkuu hujaeleza juhudi zako zimekwamia wapi zaidi ya kutaja elimu? Watu wengi wakisoma wanakuwa na mategemeo kupita kiasi lakini wanakosa malengo na mpango wa kutimiza malengo.
 
Wasomi bado ni watumwa kwa wanasiasa- Joh Makini (Karibu tena kwenye show za Joh)
 
Nimekaa na kufikiri namna ambavyo wasomi wa Taifa hili tulivyolisaidia Taifa letu. Nimekuja kugundua na kuhitimisha kuwa elimu tunayopata darasani, iwe katika nchi za wenzetu au masomo ndani ya nchi, hayanufaishi Taifa (Nitaelezea mda nikipata)

Katika safari yangu ya masomo ya miaka 27 (ukiondoa elimu ya Musingi na Sekondari) katika nchi, za Scandinavia, Pacific na Urusi ya zamani kwa kazi ninayofanya haijafikia hata 1/8 ya elimu niliyonayo kichwani mwangu. Ni kweli tunaona dhamira chanya ya Mh. Rais ya kulipeleka Taifa katika uchumi wa kati. Hata hivyo, je ni kwa kiasi gani Serikali inawawezesha wasomi wa nchi hii kuipeleka nchi katika huko tunakokutaka (uchumi wa viwanda)? Aslani ni kwa kiasi kidogo sana. Kwa nini wasomi tutumie rasilimali nyingi [ikiwemo muda wa miaka mingi kusoma masomo magumu nje ya nchi na hata ndani ya mipaka ya nchi] na baada ya hapo ukirudi nchi hainufaiki na tulivyovisoma nchi za wenzetu!!!! Ni hatari sana.

Kuna rafiki yangu Mturuki nilikuwa nikisoma naye Scandinavian Academy of Aeronautics [Gothenburg], nitatumia jina la Kaplan] siyo jina lake halisi. Kaplan alikuwa akisoma 'combustion engineering technologies' na mimi nikisoma Aeronautical Engineering aliwahi kinieleza kuwa kutokana na elimu yake aliyoitafuta kwa muda wa miaka minane katika eneo hilo la 'combustion engineering technologies' nchi yake itanufaika vilivyo kwa kodi atakayoilipa kutokana kiwanda chake cha injini atakachokianzisha baada ya kuhitimu masomo yake. Nilistaajabu kwa kauli hiyo kwa kuwa jamaa nilikuwa nikimjua maisha yake kwa muda wa miaka mitatu mfululuzo na hatakuweza kutabiri maisha ya wazazi wake kule nyumbani kwao kuwa hayatofautiani sana na maisha ya wazazi wangu nyumbani kwetu Tanzania. Ndiyo, nilikuw sawa kwa kadiri ya naelezo ya bwana Kaplan nikifananisha ya maisha ya nyumbani kwetu Tanzania. ........ Miaka minane baada ya kumaliza masomo yake ndoto ya Kaplan ilikuwa imetimia huku akiwa na harakati za kujenga viwanda vingine katika nchi za jirani.
Je mimi katika safari yangu ya miaka 27 niko wapi? Je kwa nini niko hapa?
***** Nitaendelea kuwaelezea.
Muendelezo vipi sasa
 
Mturuki ana vinasaba tofauti na wewe hatakama mna kiwango cha elimu kinachofanana,

Mturuki yuko kwenye mazingira ambayo ni rahisi kupata funds za kuanzisha startup co,

mturuki anajua akilipa kodi kesho yake tu inarudi mtaani kuboresha huduma za jamii yake ikiwemo na kuongeza mishahara ya wafanyakazi tofauti na wewe ukilipa kodi kesho utasikia imeenda kujenga airport isiyo na lila wala fila,

anyway, tunasubiri muendelezo wako.
 
Back
Top Bottom