GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Nilipokuwa "mdogo", niliaminishwa kuwa wasomi si wanasiasa na hata wakiwa kwenye siasa husimamia misimamo yao ya kisomi.
Lakini baada ya kuanza kufuatilia mambo ya kisiasa, nilibaini kuwa si wasomi wote wanaoweza kusimamia misimamo yao nyakati zote, hasa misimamo yao inapohatarisha "ugali" wao.
1. Wakati akiwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Dr. Mwakyembe alisimamia msimamo wa muundo wa Serikali tatu, lakini alipolamba shavu la ujumbe wa Bunge maalum la Katiba, alihama kutoka Serikali tatu hadi mbili.
2. Wasomi wa Sheria kutoka vyuo Vikuu 15 nchini waliandika kitabu wakielezea msimamo wao juu ya muundo sahihi wa Muungano. Walipendekeza muundo wa Serikali tatu kuwa ndiyo mwarobaini wa kero za Muungano. Lakini walipoingia kwenye bunge la katiba, wakawa watetezi wa Serikali mbili.
3. Wakati wa utawala wa Magufuli, kulipoibuka ugonjwa wa corona, wanasiasa wengi walimuunga mkono kwa kupigia chapuo ufukizaji kama njia ya kujikinga na corona badala ya kutumia chanjo ya Wazungu. Lakini alipofariki, na dereva mwingine kukamata usukani, nyimbo zao nazo zikabadilika kulingana na matakwa ya dereva. Kufukiza kulikejeliwa na chanjo ya Wazungu ikapata wapambaji.
4. Aliyewahi kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (sikumbuki jina lake), baada ya Uchaguzi wa 2020, alisema kuwa Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki. Lakini baada ya Magufuli kuaga dunia, alipohojiwa na BBC, alidai kuwa Uchaguzi ulikuwa na mapungufu.
Inaonekana majibu yake ya awali aliyasema, si kwa utashi wake , bali alisukumwa na uwoga kama si unafiki.
Huyo ni Mwalimu wa Chuo Kikuu lakini ni mwoga!
Kama wasomi wanapaswa kuwa jasiri, lakini Mwalimu wao ni mwoga kiasi hicho, unatarajia wanafunzi wake waweje? Siyo kwamba nao watakuwa "wanafiki" kama walimu wao?
5. Sijafuatilia misimamo ya Dr. Bashiru Ally, Profesa Kabudi, Humphrey Pole Pole, n.k. kabla na baada ya kulambishwa asali kama iliendelea kubaki kama hapo awali, kwa hiyo hao sitawazungumzia.
Mifano ni mingi. Na inafikirisha. Baadhi ya wanaojulikana kama wasomi wako kama vile akili zao zinaendeshwa na mtu mwingine kwa kutumia "remote control".
Pongezi nyingi ziwaendee baadhi ya wasomi na viongozi wa kada mbalimbali ambao katika nyakati tofauti, wameonesha kutokuyumbishwa juu ya kile wanachokiamini.
Watu kama hao ndiyo wanastahili kuitwa wasomi na viongozi.
Miongoni mwao ni pamoja na:
1. Jaji Joseph Warioba
2. Tundu Lissu
3. Dr. Charles Kitima
4. Profesa Issa Shivji
5. Dr. Benson Bagonza
6. Askofu Josephath Gwajima
7. Joseph Butiku
8. Askofu Severine Niwemugizi
9. Amani Abeid Karume
10. Lazaro Nyalandu
11. Othman Masoud
12. Fatma Karume