Japhari Shabani (RIP)
R I P
- Jan 16, 2007
- 721
- 178
Wasomi waamua kumuanika Makamba
Thobias Mwanakatwe
Mtandao wa Wasomi na Wataalam Mkoa wa Mbeya, umemshambulia Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na kumuonya kuacha kuingiza porojo na utani anapojibu hoja za msingi zinazowagusa Watanzania kwani anakiweka chama katika wakati mgumu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani.
Mtandao huo ulitoa kauli hiyo katika mkutano na waandishi wa habari jana, kuelezea kauli ya Makamba aliyoitoa Ijumaa iliyopita alipoitisha mkutano kujibu mapigo dhidi ya taarifa zilizoripotiwa katika kongamano la Mwalimu Nyerere lililofanyika wiki iliyopita.
Katika kongamano hilo, vyombo vya habari kadhaa viliripoti kwamba baadhi ya watu wanashauri kuwa Rais Jakaya Kikwete atoswe kwa vile anasita kufanya maamuzi magumu ndani ya chama hicho.
Mwenyekiti wa mtandao huo, Prince Mwaihojo, alisema tatizo la Makamba ni kupenda kuingiza porojo na utani wakati wa kujibu hoja za msingi ambazo zinaelekezwa kwa chama na serikali hali ambayo imesababisha wananchi na viongozi kutokuwa na imani naye.
Mwaihojo ambaye ni mwanachama wa CCM mwenye kadi namba 725928 aliyoikata mwaka 2000 katika tawi la CCM Ghana, jijini Mbeya, alisema Makamba ni mzigo kwa chama kutokana na kila mara kuingiza porojo na utani hata katika mambo ya msingi ambayo yanakuwa yanalalamikiwa na Watanzania.
Makamba ajibu hoja: hakuna Mtanzania asiyefahamu kuwa Rais Kikwete amekuwa mgumu katika kuchukua maamuzi dhidi ya wanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi, na hayo ndiyo malalamiko ya msingi aliyopaswa kuyajibu na siyo kuingiza porojo zake ambazo tumezizoea, alisema Mwaihojo.
Mwaihojo ambaye aligombea ubunge uchaguzi wa 2005 katika Jimbo la Mbeya Mjini kupitia CCM na kuangushwa kwenye kura za maoni, alisema Makamba ni miongoni mwa viongozi ambao hawatambui dhamana na thamani ya nafasi walizonazo katika chama na umma na ndiyo maana hawana mtazamo mpana wa kujua kwa sasa Watanzania wanataka nini.
Makamba asiwe mropokaji awe anajenga hoja na kujua nini umma wa Watanzania unataka, anawaondoa watu kwenye hoja za msingi analeta vichekesho na porojo, hii ni dharau kwa wananchi na kuwafanya hawana akili, alisema Mwaihojo.
Mwenyekiti huyo alisema udhaifu wa kiutendaji unaoonyeshwa na Makamba, ndiyo umeanza kusababisha umaarufu wa CCM kuanza kuporomoka taratibu kadri siku zinavyoendelea ikilinganishwa na miaka ya nyuma hali ambayo kama chama hakitachukua tahadhari Uchaguzi Mkuu wa 2010 utakuwa mgumu kwa chama hicho.
Alisema chama kinapaswa kujiuliza mara kadhaa hivi kuendelea kuwa na kiongozi kama Makamba kitapiga hatua kimaendeleo au kitadidimia kwa sababu kuwa kiongozi ndani ya chama kikogwe kama CCM, lazima mtu awe makini anapojibu hoja na malalamiko yanayotolewa na Watanzania ambao ndio wanakiwezesha chama kiendelee kushika hatamu ya uongozi.
Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa iliyopita, Makamba alidai tuhuma dhidi ya Rais Kikwete zinatolewa na watu wenye visasi, walioshindwa uchaguzi na ambao wanafadhiliwa na matajiri wale wale wanaoitwa mafisadi wa CCM.
Makamba alidai tuhuma hizo zimejengwa katika misingi ya chuki kwani wengi wa makada wa chama hicho waliokuwa wakizungumza katika kongamano hilo, ama wao wenyewe au wagombea wao waliangushwa katika harakati zao za kisiasa huko nyuma.