Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,422
- 5,659
Soko la ajira hivi sasa ulimwenguni kote linakabiliwa na ushindani mkubwa, kwani nafasi ni chache na wenye uhitaji ni wengi. Tanzania kama zilivyo nchi nyingi duniani tunakabiliwa na tatizo la ajira kwa watu wetu hasa vijana ambao ni kundi kubwa zaidi na zalishi linalounda idadi ya watu wetu zaidi ya milioni 61.
Kuna njia kuu 4 za kutatua tatizo la ajira nazo ni;
I) Kubadili mfumo wa elimu
II) Kuwainua walioamua kujiajiri
III) Kubadili mbinu za uajiri
IV) Serikali kuandaa sera bora ya elimu
Tatizo la ajira nchini kwetu linachagizwa na changamoto kuu mbili ambazo ni:-
A) Ujuzi tunaoupata katika mfumo wa elimu yetu kutoendana na vigezo vinavyotakiwa katika soko la ajira.
B) Upatikanaji mgumu wa mitaji na gharama za kuendesha biashara ndani ya nchi kuwa kubwa.
Tunaelewa kuwa suala la ukosefu wa ajira na changamoto zake si suala rahisi kulimaliza kwa mara moja aghalabu tunaweza kupunguza tatizo kwa kwa kuboresha baadhi ya mambo kadhaa katika elimu yetu.
Nimebaini kuwa tatizo kubwa linalowakabili wahitimu wengi wasiweze kuajirika ni pamoja na kutokuwa na umahiri wa ziada katika nyanja mbalimbali za ujuzi ambazo ni matamanio makubwa ya waajiri walio wengi.
1. Ujuzi kwa vitendo
Hiki si kipindi cha mhitimu kubakia na ujuzi wa aina moja tu ule aliousomea katika vyuo vikuu bali anaweza kujiongezea ujuzi katika fani zingine ikiwemo kujifunza ufundi, udereva, utengenezaji wa bidhaa mbalimbali, kujipatia ujuzi katika kilimo na ufugaji, kusindika, kushona.
2. Ujuzi usioshikika (soft skills)
Mhitimu ahakikishe kuwa anajipatia kazi ya kujitolea hata kama ni bila malipo ilimradi aweze kujipatia ujuzi huu ambao haupatikani pasipo kuwa maeneo ya kazini na kuendelea kuzoea taratibu taratibu.
Faida zake ni pamoja na; kujijengea uwezo wa kutatua changamoto, kutoa maamuzi, kuwa kiongozi, kuweza kujiongoza, ustahimilivu, kufanya kazi kwa ushirikiano, uwezo mzuri wa kuwasiliana, kufuata maadili ya kazi na unyumbulifu.
3. Ujuzi wa kidigitali
Hili ni suala mtambuka ambalo linaingiliana na vipengele vyote vya ujuzi kwa kuwa ni daraja katika kujijengea uwezo wa ufikiaji, usimamiaji, uelewa, uhusanishaji, uwasilishaji, uchambuzi na utengenezaji taarifa salama na itajika.
Mbali na kuwa asilimia kubwa ya wahitimu huwa na uelewa wastani katika programu muhimu za kiofisi (Ms Office) mhitimu anayeitaji kumudu ushindani anapaswa kujiendeleza zaidi katika software za aina mbalimbali ikiwemo mobile computing, enhancing work output, conferencing & search expertise, uchakataji data na mitandao ya kijamii.
4. Uwezo wa kujamiana na jamii zenye tamaduni tofauti (intercultural capacity)
Msomi mzuri ni yule aliyeelimika kiasi cha kutambua kuwa nje ya tamaduni za jamii yake anapaswa pia kuheshimu na kuzitambua imani na dini za watu wengine wasio amini kama yeye na kuwapa uhuru na haki wanayostahili kufuata kile wanachoamini na kukiishi.
5. Uwezo wa kuzungumza na kutumia lugha zaidi ya moja
Waajiri uhitaji wafanyakazi wanaoweza kuboresha mawasiliano katika eneo la kazi na kuweza kufikia ufanisi mzuri wa maelewano, kuokoa muda na kuepusha gharama zisizo za lazima.
Mfanyakazi wa namna hii uvutia waajiri kwani nirahisi kujenga mahusiano na wafanyakazi wenzake, kuongea na watu wa mataifa mbalimbali kufanikisha shughuli za kibiashara, kujenga mtandao na mahusiano.
Pendekezo langu kwa Serikali; Ianzishwe programu maalumu ya mafunzo ambayo itaangazia katika mambo makuu matatu ambayo ni Lugha, Kompyuta na Udereva kwa mhitimu wa kidato cha sita kabla ya kujiunga na mafunzo ya elimu ya juu.
Mhitimu yeyote wa kidato cha sita asiruhusiwe kuendelea na masomo ya chuo kikuu pasipo kupitia mafunzo husika katika vyuo maalumu vya umma na binafsi ambavyo vitakuwa vimeidhinishwa na vitatoa vyeti halali kwa madaraja kulingana na ufaulu wa mwanafunzi katika kozi husika.
Serikali iandae miundombinu bora ya kujifunzia, vifaa na walimu wabobevu kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kufanikisha hili katika ufanisi na ubora wa juu.
1. Lugha
Mkazo uwe katika kujifunza lugha walahu mbili ambapo kujifunza kingereza iwe ni lazima na lugha nyingine ya kimataifa (1) iwe ni chaguo la mwanafunzi kulingana na machaguo yaliyopo.
Kwa kuzingatia kuwa watanzania wengi wanafahamu kiswahili kwa ufasaha ambayo pia ni lugha ya kimataifa kwa kuongezea na lugha nyingine mbili za kimataifa itatufanya tuwe na idadi kubwa ya wasomi na kizazi kitakachoweza kuzungumza lugha zaidi ya mbili.
Hii ni faida kubwa katika kufungua milango ya fursa za ajira, utalii, biashara na uwekezaji, kupambania nafasi za udhamini wa kimasomo (scholarships) kuboresha mahusiano na nchi mbalimbali pamoja na kuambukizana ujuzi, teknolojia na maarifa katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa urahisi zaidi.
2. Kompyuta
Tunahitaji kuandaa wasomi watakao acha alama baada ya masomo yao ya vyuo vikuu ikiwemo machapisho mbalimbali ya kitaaluma, tafiti na vumbuzi.
Kwa kufanya hivi tunawaandaa vijana wetu kuingia vyuo vikuu wakiwa tiyari na sifa ya ziada itakayowasaidia katika kuandaa na kuwasilisha ripoti zao, tunawapa sifa ya ziada kwa waajiri wao, lakini pia serikali itanufaika nao kwa kuwa na wafanyakazi bora wenye ujuzi katika TEHAMA.
Vyuo vitaongeza idadi ya machapisho ya kitaaluma kwa njia ya mtandao na nakala ngumu ambayo kwa namna moja husaidia katika kupandisha ubora na thamani ya elimu yetu lakini pia kupitia tafiti mbalimbali zitakazofanyika nchi yetu itanufaika zaidi na wasomi wake.
3. Udereva
Vyuo viwe na magari ya kujifunzia na gereji kwa ajili ya mafunzo ya awali ya ufundi magari, mhitimu apewe leseni ya udereva yenye madaraja ya awali.
Manufaa ya kuwapatia vijana wetu mafunzo ya udereva ni kuandaa jamii iliyostaarabika itakayokuwa na ufahamu juu ya sheria za usalama barabarani na udereva mzuri wa kujihami, ujuzi, kupunguza gharama zisizoitajika kwa waajiri, kuongeza ufanisi katika usimamizi wa vyombo vya moto vya umma na sekta binafsi.
Katika ngazi ya vyuo vikuu kwa faculty zote ziwe ni za elimu, jamii, sayansi, teknolojia, sanaa,n.k suala la kujifunza na kufanya tafiti kabla ya kuhitimu liwe ni jumuishi na litiliwe mkazo kwa maana tuna uhaba mkubwa wa machapisho ya kitaalamu, makala, vitabu n.k
Hii inapelekea elimu yetu ikose rejea hata kwa vizazi vilivyopo na vijavyo huku tukitengeneza kundi kubwa la wasomi tegemezi na wanyonyaji wa maarifa yaliyoandaliwa na wengine, wasio na uthubutu, ushauri wala maarifa ya kuja kubaini baadaye maeneo yenye mapungufu ya kufanyiwa marekebisho au kuboreshwa katika sera, sheria, mazingira yao na kazi watakazopewa kufanya.

Upvote
1