Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Jukwaa la JF
Wito wangu ni kwa mamlaka ya nchi na Wataalamu wa Afya wafanye yafuatayo ili kuwa na uwezo wa kujikinga na kupambana na magonjwa mbalimbali:
1. Mamlaka ya nchi iwezeshe kifedha wataalamu wa afya na sayansi kwa ujumla kufanya utafiti wa uwezekano wa kutengeneza chanjo ya magonjwa mbalimbali yanayosumbua afya za wananchi;
2. Wasomi wa sayansi, wataalamu na madaktari wa afya wakutane haraka wakishirikisha na taasisi za utafiti kama NIMR, COSTECH , Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC), African Medical and Research Foundation (AMREF), Ifakara Health Research and development Centre (IHRDC), Mwanza Medical Research Centre (MMRC), Amani Medical Research Centre, Tukuyu Medical Research Centre nk wapange mikakati yenye tija kutafiti tiba na chanjo ya magonjwa mbalimbali.
Tanzania ina wasomi wengi sana na ambao wamebobea kwa yakini katika taaluma ya kuaminika . Madaktari waliosomea huko Cuba, Urusi, China, Ulaya, nk watumie taaluma yao kwa manufaa ya wananchi ambao ndio wateja wa uhakika kwa gharama nafuu. WAKUMBUKE AHADI HII: "Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumikia elimu yangu kwa faida ya wote"
3. Wananchi wajengewe hali ya kujiamini na kuondolewa HOFU maana ndicho kichocheo cha afya kunyong'onyea hatimaye magonjwa mengine nyemelezi kuchukua nafasi kushambulia.
Wenye fikra za kisiasa wakichangia mada hii wataharibu ni bora wakae pembeni wawaachie wataalamu na wenye mawazo chanya tu.
Karibu