Jumuiya ya Umoja wa vijana wa CCM Taifa chini ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa Vyuo na Vyuo Vikuu Ndg. Mohammed Ali Kawaida inatarajia kufanya Mkutano mkuu maalum wa UVCCM Vyuo na Vyuo vikuu utakaokutanisha Viongozi wote wa mikoa yote wa vyuo na vyuo vikuu mkoani Dodoma tarehe 16 Machi, 2025 saa mbili asubuhi, katika ukumbi wa NEC - CCM Makao Makuu.
Mgeni Rasmi katika Mkutano mkuu huo anatarajiwa kuwa Ndg. Mohammed Ali Kawaida MCC) Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM na Mlezi wa Vyuo na Vyuo Vikuu Tanzania
Kauli mbiu ya mkutano huo mkuu maalum wa vyuo na vyuo vikuu ni; ”Wasomi tumekuelewa Dkt Samia Suluhu Hassan, Maendeleo tumeyaona, Dkt Samia Mgombea wetu 2025”
Wajumbe wote wa mkutano mkuu maalum wa vyuo na vyuo vikuu tunawakaribisha Dodoma.