Wassira amgomea JPM, asema halipi deni la Commodity Import Support. Akataa wito, Task Force kutuma Polisi. Yeye adai yuko tayari kupigwa pingu!

Wassira amgomea JPM, asema halipi deni la Commodity Import Support. Akataa wito, Task Force kutuma Polisi. Yeye adai yuko tayari kupigwa pingu!

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Kumekucha!

Steven Wasira,mmoja wa wadaiwa sugu wa mfuko wa Commodity Import Support amesema hatalipa deni hilo kamwe na kwamba yeye si mmoja wa wadaiwa wa mabilioni hayo.

Wasira ambaye anakiri kukopa milioni mia moja miaka ya tisini,anasema alikuwa na makubaliano ya kulipa benki ya T.I.B, na kwamba makubaliano hayo yalifanywa wakati Mkurugenzi wa Benki hiyo,na mtuhumiwa wa ufisadi,bwana Peter Noni akiwa mamlakani.

Cha ajabu,Benki hakuna kumbukumbu za kulipa deni kama Wasira anavyosema alilipa, na hana hata barua ya Benki kuonyesha kwamba imethibitisha kwamba kalipa na hadaiwi, wasira ana maneno tu hana documents za benki kuonyesha uthibitisho kwamba hadaiwi,je mchezo ulichezwa hela ikarudi kwa wasira,hivyo Wasira anaweza kuwa ametakatisha pesa?

Muda wote anaimba "noni,noni,noni"

Je Wasira na kundi lake la awamu ya tano walikuwa wanashinikiza na kuwatisha watendaji wawafutie madeni yao kiaina? Anasema aliachana na kampuni iliyokopa akaenda kufanya siasa,sasa kwa nini Benki au yeye aambiwe na Benki aiandikie ili ifute deni wakati yeye si mtumishi wa kampuni ya SIZYA COLD STORAGE?

Wasira alikopa milioni 100 miaka ya tisini,anataka alipe hizo pesa hivyo hivyo bila riba! Amekopa miaka 30 iliyopita?!

Haiwezekani, akamatwe na apewe kesi ya uhujumu uchumi,tena anamgomea Rais wa Jamhuri ya Muungano ! Anajiamini nini huyu mtu?hajui hii ni awamu ya tano!

Asomeshwe namba,
 
Hata sijaelewa kwa jinsi ulivyoiandika hiyo habari yako.
Ila kwa kidogo nilicho kieleqa alipe tu, hakuna kucheka na nyani.
 
Linapokuja suala la kupambana na wakwepa kodi automatically nakuwa upande wa JPM
Mkuu asikupoteze Huyo JPM, hivi kule kwenye dini Lucifer ana weza kukuandalia makao mbinguni?
Ili watu washughulikiwe uporaji wao inabidi kuiondoa CCM madarakani kisha sheria (ambayo ipo siku zote) ifuate mkondo. Huyo unayesema uko upande wake ndio hatari zaidi.
 
Maigizo tu. Zile trilioni moja unusu ambazo baadaye zikabainika ni trilioni mbili pointi nne, na latest figure ni ni trilioni nne nukta nane mbona amezikalia kimya? Kisa mhusika ni mpwae Doto? Ya LUGUMI yameishia wapi?

Na kesi ya vipusa ya kaka yake Rostam ilikwishaje?
Linapokuja suala la kubana wabadhilifu na washenzi nakuwa na JPM upande mmoja
 
Back
Top Bottom