Wassira amgomea JPM, asema halipi deni la Commodity Import Support. Akataa wito, Task Force kutuma Polisi. Yeye adai yuko tayari kupigwa pingu!

ni kulipa tu maana hamuna nam
 
Hao ndio wana siasa wa Tanzania. Wengi ni wezi kweli kweli wa mali ya umma. Ndio maana majungu na fitna yamekuwa msingi wao imara wa kuendelea kushiriki siasa. Hawana kipya cha kuongeza.
 
Yaani hizo milioni 100 alizokopa ndizo alizowekeza kwenye kale kamradi ka kuuza samaki? Kale kamradi hakakuwa hata na thamani ya milion 2!!
 
Linapokuja suala la kupambana na wakwepa kodi automatically nakuwa upande wa JPM
Kwasababu na wewe ni "Mkwepa Kodi" chuma kitakupitia kama bullet lipa kodi ili uwe mtoto pendwa
 
Mzee wetu jamani. Ameifanyia nchi mengi mema hiyo yaweza kuitwa, Posho yake tu. Tumsamehe. Lakini jinsi hili jeshi lilivyokosa utu, kweli wanaweza kumtia pingu. Ole wenyu mkamatwe na Tspca
 
Alipe tu pesa za wananchi. Aache kutapatapa dawa ya deni ni kulipa siyo kuonewa huruma.
 
Magamba yanapoburuzana, teh teh
 
Linapokuja suala la kubana wabadhilifu na washenzi nakuwa na JPM upande mmoja
Angeachana na yale matakataka mengine yote, ni nani angepinga juhudi zake hizi?

Angekuwa na haja gani tena ya kuhangaika na hao wapinzani ambao hata sera zao hazijulikani? Huko kwenye kukiuka na kukanyaga haki za wengine hakuwa na sababu kabisa ya kupaingia.
Mavitu anayojenga, kupigania maslahi ya taifa, ni mTanzania gani asiyevitaka hivyo?

Kwa nini ukahangaike na vitoto vinavyohoji PhD? Inasaidia kitu gani kama matendo unayofanya yanazidi hizo PhD mara milioni?

Angejikita ndani ya kufanya mambo ndani ya 'taratibu' na kama ingebidi kukiuka mara chache sana kwa sababu maalum, watu wangeelewa tu na kubaki nae. Hata Katiba iwe makaratasi tu kwa utashi wa mtu mmoja? Hapana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…