Wassira amgomea JPM, asema halipi deni la Commodity Import Support. Akataa wito, Task Force kutuma Polisi. Yeye adai yuko tayari kupigwa pingu!


Huenda unabeba mambo kwa kufuata mkumbo ndio maana umetekwa na kwamba watu wanapinga kila kitu. Ni vyema ukajiridhisha watu wanapinga au kukosoa nini na zipi hoja zao. Lakini ukija na mtazamo na hii propaganda mfu ya kwamba watu wanapinga kila kitu basi hutaelewa chochote.

Huenda nyie ndio mnaomwambia kwamba watu wanapinga kila kitu, ndio mnaopotosha na yeye anaamini anapingwa kwa kila kitu. Unasema eti akionyeshwa chuki na yeye ataonyesha chuki, kwanza yeye sio Mungu bali ni binadamu mwenye madaraka ya muda tu. Na kama ni chuki basi ujue alikuwa nayo since day one kwani sio kiongozi wa kipawa bali mfumo mbovu ndio uliombeba. Hakuna mtu anayesema kila kitu anakosea kwani hakuna binadamu wa hivyo, bali visasi na chuki yake dhidi yetu iwazi.
 
Jambo gani jpm kafanya kisha likaungwa mkono 100% na wapinz@ni? Nisaidie mkuu...
 
maana yako iko very naked mkuu haitaji kutumia akili kubwa.

Huwezi kumwita SOKWE binadamu mwenzako
Nasisitiza, hakuna mtu aliyeitwa sokwe. Ila kama unataka kutafsiri hivyo ni maoni yako, pengine wewe unataka kumuita mtu sokwe?
 
Jambo gani jpm kafanya kisha likaungwa mkono 100% na wapinz@ni? Nisaidie mkuu...
Na kwa nini liungwe mkono 100%, not any other percentage? By the way, Lissu amewahi kuunga mkono kwa 100% juhudi za Rais Magufuli kutufundisha kuwa haki za binadamu, utawala wa sheria na demokrasia ni muhimu sana.
 
Makada wa Chama pendwa ndy wanaongoza kwa kujichotea mpunga

Ova
 
kweli wewe kinembe, hii taarifa umeitoa wapi? kumbuka dua ovu haiunguzi nyumba,
 
Wewe katika hili upo upande gani? Wasira au selikali?
 
Kumekucha wacha WAPARURANE! Ndipo hapo Wassira atarudisha mashambulizi ya nguvu tena hadharani kuelekea kwa nduli na Watanzania KULIPUKA kwa furaha.

 
Yaani kuna watu hata kifanyike nn nchini yeye anapinga...jamani!!!! What's wrong? Ni laana au? Ninyi baadhi ya watu wa upande wa pili mna matatizo gani?
Wewe ndio ujiulize unashida gani?
Ukimwaga mboga na ugali umwagwe.
 
Jambo gani jpm kafanya kisha likaungwa mkono 100% na wapinz@ni? Nisaidie mkuu...

Ukikuta mtu kafanya jambo akaungwa mkono kwa asilimia mia moja ujue hiyo jamii imepoteza uwezo wa kufikiri. Halafu mimi sio msemaji wa upinzani.

Labda ungeniluliza mimi namuunga mkono kwenye yapi. Elimu bure hili namuunga mkono ila angeenda mpaka form 6, kisha huko vyuoni watu wapate mikopo. Kutokukatika hovyo kwa umeme kwa eneo nililopo. Kuwatimua Nape na mwigulu uwaziri kwani ni watu waliopandikiza siasa za ukatili na hila na sasa yeye anaziendeleza.

Simuungi mkono kwenye ununuzi wa ndege kwa sasa kwani ni biashara Mtambuka, bali alipaswa awekeze kwenye kilimo cha umwagiliaji au kujenga viwanda wangalau kila mkoa au kila kanda vya 30b-50b vitoe ajira kwa vijana. Kwa hiyo kwamba anapingana kila kitu ni lugha ya upotoshaji. Ufahamu hata saa mbovu kuna wakati inasema sawa.
 
Je linapokuja suala la CAG kupunguziwa bujeti ili asifanye ukaguzi kwenye matumizi ya hovyo ya sirikali WEWE UNAKUWA UPANDE wa nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…