Wassira, Chikawe, Lukuvi kikaangoni kuhusu Katiba

Wassira, Chikawe, Lukuvi kikaangoni kuhusu Katiba

KALOKAZA

Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
95
Reaction score
135
JK awatibulia Wassira, Chikawe

• Filikunjombe asema wanapaswa kuwaomba radhi wananchi

HATUA ya Rais Jakaya Kikwete kukutana na viongozi wa vyama vya siasa vyenye wabunge na kuridhia muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba urejeshwe bungeni, imeungwa mkono na wengi, huku mawaziri wake wakisutwa.

Mawaziri hao ni Stephen Wassira (Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu), Mathias Chikawe (Katiba na Sheria) na William Lukuvi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge).

Kwa nyakati tofauti baada ya vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi, kususia muswada huo bungeni waliwakejeli wakidai kuwa wanapoteza muda kwani safari hii hakuna nafasi ya kukutana na Rais Kikwete kama ilivyokuwa awali mwaka 2011.

Mawaziri hao waliongeza kuwa viongozi wa upinzani wanatamani kwenda Ikulu kunywa chai na juisi, huku wakisisitiza kuwa milango hiyo sasa imefungwa na rais lazima asaini muswada huo kama ulivyopitishwa na Bunge, kwamba kutofanya hivyo ni kutangaza mgogoro na wabunge.

Licha ya kejeli hizo, Rais Kikwete aliamua kukutana na viongozi wa vyama hivyo vitatu jana huku akiwashirikisha pia wale wa CCM, TLP na UDP ambao wabunge wao waliupitisha muswada huo.

Akizungumza jana na gazeti hili, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), alimpongeza rais kwa hatua hiyo na kumtahadharisha awe makini na wabunge wa chama hicho, akidai wamekuwa wakitumia wingi wao vibaya bungeni.

Filikunjombe alisema Kikwete ameonesha ukomavu na kwamba hiyo ndiyo demokrasia ya kuwasikiliza wachache pia.

“Kwenye katiba hakuna mshindi, muswada uliopitishwa si wa CCM, katiba si ya CCM, inapaswa kuwa ya wananchi wote hata wachache wasikilizwe.

“Katiba mpya haikuwa ajenda ya CCM, rais aliichukua labda kutoka chama kingine akaona inafaa. CCM wamepokea suala la mabadiliko ya katiba bila kukubali maumivu yake, ndiyo maana tunafikia hatua hii,” alisema.

Alifananisha hatua hiyo na mtu unayetaka kufika mbinguni halafu hutaki kufa, hivyo kuwataka wenzake wakubali mabadiliko na maumivu yake.

“Mimi ninamtia moyo Rais Kikwete asimamie vizuri suala la katiba, ila ajue wabunge wengi wa CCM tunamharibia, awe makini na sisi, kwani mara nyingi tunatumia wingi wetu vibaya.

“Imekuwa aibu sasa mara ya pili rais anarejesha muswada kufanyiwa marekebisho, ingefaa wabunge wa CCM tujitafakari, sisi tunamtumikia nani?”alihoji.

Filikunjombe aliongeza kuwa katika hilo Kikwete ameonesha amedhamiria kwa dhati kuusimamia mchakato, hivyo aungwe mkono.

Akizungumzia kauli za kejeli za mawaziri, mbunge huyo machachali alisema hao wana akili mgando tu, yafaa wawaombe radhi Watanzania.

“Na hii ni kwa sababu hapa kwetu utamaduni wa kujiuzulu haupo, lakini vinginevyo hizo si kauli za kusemwa na mawaziri,” alisema.

Alipotafutwa Waziri Wassira, kuelezea msimamo wake baada ya mazungumzo ya rais na viongozi wa vyama, alijibu kwa kifupi akiomba aulizwe Waziri Chikawe, kwa maana kwamba yeye hakuwa na la kusema.

Waziri Chikawe naye alipotafutwa, aliomba apigiwe simu baadaye kwa maelezo kuwa hakuwa katika nafasi ya kuzungumza kwa wakati huo.

Ndugai asahau kanuni
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambaye alisimamia ubabe wote bungeni hadi muswada kupitishwa na kasoro hizo, alipotafutwa alionesha kushangaa, kwa maana kuwa hajui wapinzani wanabishania nini na walikwenda kumuona rais kwa suala lipi.

“Ni issue (suala) gani hasa ambayo inahitaji udharura wa aina hiyo, unaposema wataurejesha muswada katika Bunge lijalo, je, kanuni zinaruhusu?

“Mimi sioni mantiki yoyote, labda wanaozungumza hoja ya uteuzi wa wajumbe 166, kama rais hataki hilo ni suala jingine, ila sisi tuliona rais ndiye chombo kinachofaa kuchuja wajumbe hao,” alisema.

Kwa mujibu wa Ndugai, bila mamlaka ya kuchuja wanaweza kujikuta wana wajumbe wa kutoka kanda, dini au jinsia moja, kwamba mamlaka ya kuchuja inahitajika.

Kuhusu muswada kurejeshwa bungeni, Ndugai alisema hana uhakika kama utarejeshwa, ila anachofurahi yeye ni kusikia kuwa muswada umesainiwa.

CCM wakubali
Chama Cha Mapinduzi kupitia kwa Katibu wake wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema Rais Kikwete kwa kusaini inaonesha anafuata sheria, lakini pia wanampongeza kwa kukutana na viongozi wa siasa.

Alisema kuwa yale yatakayorejeshwa bungeni, wabunge wataamua kama wakiona yana hoja wasikilize na wakiona hayana watajua wao kwa vile Bunge ni mhimili huru.

Kuhusu kauli za kejeli za baadhi ya mawaziri, Nape alisema hajui na hajawahi kusikia.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), Sadifa Khamisi, alisema Bunge ni chombo huru, hivyo litaangalia kama kuna masuala ya kubadili.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Alexanda Makulilo, kwa upande wake alisema rais ametumia busara kuwasikiliza wapinzani, kwa kuwa aliona wana hoja.

Alisema marekebisho yafanyike, wabunge sasa wakafanye majadiliano vizuri, waone umuhimu wa hoja na waweke masilahi ya vyama pembeni na kutanguliza manufaa ya nchi.

Viongozi wa dini wasifu
Baadhi ya viongzoi wa dini wamemsifu Rais Kikwete kwa hatua ya kukutana na viongozi wa vyama, kwamba kitendo hicho ni pigo kwa mawaziri ambao wameifanya Ikulu kuwa hatimiliki yao.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mwenyekiti wa kamati ya viongozi wa dini wa taaluma, maadili na haki za binadamu kwa jamii, Mchungaji William Mwamalanga, alisema Kikwete ana nia njema lakini watendaji wake wamekuwa wakimpotosha.

Mwamalanga alisema kuwa hatua hiyo ya kuwa na majadiliano ya pamoja imeonesha ujinga uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watendaji ambao wamekuwa wakitoa kauli za kukejeli wapinzani.

“Huwezi kuwa na hatimiliki ya Ikulu, hili ni lazima mawaziri Lukuvi, Chikawe na Wassira wakatambua. Maana hatua ya Rais Kikwete kukutana na viongozi hao imewadhalilisha wao mawaziri,” alisema.

Kiongozi huyo alisema kuwa watendaji hao ndio waliokuwa wakipotosha katika suala hilo na kumlazimisha asaini muswada huo haraka bila kuangalia kasoro.

Alisema kuwa ni muhimu sasa Rais Kikwete akasimamia utekelezaji wa makubaliano hayo ili malengo yaliyowekwa yakaweza kufikiwa.

Mwamalanga alisema kuwa iwapo Rais Kikwete atayaacha makubaliano hayo na kuwaachia watendaji hao kuna uwezekano wa kutokea kwa mtafaruku mkubwa ndani ya nchi katika suala hilo.
 
Ndugai,Nape,Wassira,Lukuvi ndo wanaomponza sana JK na hata ile hotuba ya mwisho wa mwezi mambo mengi ya uongo kuhusu uchochezi wa Tindu Lissu ,Jk aliambiwa na hao vilaza so kiufupi tu JK hadi washauri wake ni wapotoshaji ,elimu ndogo na wamelewa madaraka
 
sielewi kwanini Rais anaishi n a maadui zake nyumba moja.ni hatari sana kufanya kazi sambamba na akina chikawe,wasira,werema,lukuvi huku wenzie wanahujumu nia yake nzuri ya kuleta katiba mpya.
 
Mawaziri wengi wa JK wamekuwa wakifanya viroja badala ya kuwatumikia wananchi kitu ambacho JK anatakiwa aendelee kufanya nao kazi kwa tahadhari sana vinginevyo watamuingiza kwenye majanga.
 
Aibu yao hao wanaojifanya miungu watu.

Wasira hafai na amejaa jazba ndiyo maana hata watoto wote wamemkimbia na kujiunga CHADEMA chama cha watu.

Chikawe na Lukuvi aibu yao. Wanafaa kuondolewa kwenye viti walivyokalia.

Ndugai ndo kabisaa! Hata unaibu spika sijui nani alimpa. Amejaa uccm na anafuata tu upepo bila kuhusisha akili.
 
Mie nafikiri wamepitwa na wakati na ndio maana ni waiga wa MABADILIKO, Lukuvi na Wasira kamwe hawawezi kwenda na kasi ya ulimwengu wa sasa na wajue kuwa katiba sio ya kwako wala ccm kama vipi tutaidai kwa NGUVU:disapointed:
 
Ningekuwa Lukuvi au Wasira au Chikawe ningetafuta ''kamba na kamti'' kangu kulinda heshima kwakuwa Tanzania hakuna utamaduni wa kujiuzulu
 
Hapo kwa lukuvi,wasira na chikawe kuwa
wote wana akili mgando "mapoyoyo".

Fillikunjombe, you made my day kwa hilo tu!
Sikutegemea kama miccm imeanza kujitambua mmoja baada ya mwingine.
Kumbe ile habari ya ndiyoooo bila hata kufikiri nawe pia huwa inakukera ?

siku nyingine kamata mic kisha ieleze live humo humo mjengoni hakuna kupepesa macho kwa makubwa jinga hayo.
akili mgando wapeleke kuongozea familia zao na si watanzania na tanzania kwa ujumla wake.

Tumechoka kusikia takataka zenu maccm bungeni maana hoja kwenu ni sawa kujitwisha zigo la misumari.
Kweli nimeamini akili ndogo kuongoza akili kubwa ni majanga.

Halafu kwenye suala la kuomba radhi watanzania, waambie hivi watanzania hatuko tayari kupokea radhi za machizi kwani baada ya sekunde kadhaa chizi anaweza fanya tukio kubwa zaidi ya hilo. Hivyo hatuko tayari kuchezewa akili n'a hayo majanga.

Hata bwana azam atakuwa ameanza kuyajua haya ...
 
Upotoshaji wa vijana wa Bavicha unajulikana.
Nakumbuka kwa macho na masikio yangu Wassira alisema kama wapinzani wanayohoja waziwakilishe kwa Rais na waache tabia ya kukimbia mijadala bungeni, hapo ubaya uko wapi?

Lukuvi na Chikawe walisisitiza utaratibu wa kufuata kanuni na sheria na kwamba muswada umefuata taratibu zote na hauzuiliki kusainiwa.
Muswada umesainiwa, hapo ubaya uko wapi?

Marekebisho ni jambo la kawaida kwenye sheria hasa kulingana na wakati na mazingira.

Hata yaliyojadiliwa ikulu hayana tofauti na yaliyosemwa naLukivi,Chikawe na Wassira, hapo ndipo utashangaa Tundu Lisu na wenzake walikuwa wanapigania hoja gani ikiwa wamefika kwa Rais na kukubali mambo yote yaliyoko kwenye muswada na marekebisho yasiyozidi nusu paper.
 
Naanza kuelewa kwa nini Mh Kikwete anawaambia CCM wajiandae kisaikolojia, sio ajabu mwenyewe Raisi Kikwete ameona nchi haitokuwa na future ikibaki kwa CCM
 
Hawa ccm hawajui katiba hii ndio itakuja kuwalinda wao wakiwa hawatakuwepo tena madarakani!
 
Kwenye katiba hakuna mshindi, muswada uliopitishwa si wa CCM, katiba si ya CCM, inapaswa kuwa ya wananchi wote hata wachache wasikilizwe.

"Katiba mpya haikuwa ajenda ya CCM, rais aliichukua labda kutoka chama kingine akaona inafaa. CCM wamepokea suala la mabadiliko ya katiba bila kukubali maumivu yake, ndiyo maana tunafikia hatua hii," alisema.

Alifananisha hatua hiyo na mtu unayetaka kufika mbinguni halafu hutaki kufa, hivyo kuwataka wenzake wakubali mabadiliko na maumivu yake.

"Mimi ninamtia moyo Rais Kikwete asimamie vizuri suala la katiba, ila ajue wabunge wengi wa CCM tunamharibia, awe makini na sisi, kwani mara nyingi tunatumia wingi wetu vibaya.

"Imekuwa aibu sasa mara ya pili rais anarejesha muswada kufanyiwa marekebisho, ingefaa wabunge wa CCM tujitafakari, sisi tunamtumikia nani?"alihoji.
= SAFI SANA FILIKUNJOMBE, TUNATAKA WAZALENDO KAMA WEWE, NCHI IPATE MAENDELEO, HAKUNA KUUMA MANENO UKWELI UNATUWEKA HURU. LUKUVI, WASSIRA NA CHIKAWE WAPIME WENYEWE
 
lukuvi, wasira, chikawe - elimu ndogo sana. Bila ya CCM, watu hawa ni bure kabisa. Jambo moja lililo dhahiri ni ubabaishaji wao.
 
sielewi kwanini rais anaishi n a maadui zake nyumba moja.ni hatari sana kufanya kazi sambamba na akina chikawe,wasira,werema,lukuvi huku wenzie wanahujumu nia yake nzuri ya kuleta katiba mpya.

hao sio maadui wake.huwa wanakubaliana kwanza.ila kikinuka jk huwa anawageuka.hizi ni sarakasi za ccm.
 

Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM)
,
  • Wabunge wa CCM wamekuwa wakitumia wingi wao vibaya bungeni.
  • Kikwete ameonesha ukomavu na kwamba hiyo ndiyo demokrasia ya kuwasikiliza wachache pia.
  • Kwenye katiba hakuna mshindi, muswada uliopitishwa si wa CCM, katiba si ya CCM, inapaswa kuwa ya wananchi wote hata wachache wasikilizwe.
  • Katiba mpya haikuwa ajenda ya CCM, rais aliichukua labda kutoka chama kingine akaona inafaa.
  • CCM wamepokea suala la mabadiliko ya katiba bila kukubali maumivu yake, ndiyo maana tunafikia hatua hii.
  • Imekuwa aibu sasa mara ya pili rais anarejesha muswada kufanyiwa marekebisho, ingefaa wabunge wa CCM tujitafakari, sisi tunamtumikia nani?
  • Kikwete ameonesha amedhamiria kwa dhati kuusimamia mchakato, hivyo aungwe mkono.
  • Chikawe, Wassira na Lukuvi wana akili mgando tu, yafaa wawaombe radhi Watanzania.
  • Na hii ni kwa sababu hapa kwetu utamaduni wa kujiuzulu haupo, lakini vinginevyo hizo si kauli za kusemwa na mawaziri.

.
Sawa, tutakutana kwenye vikao vyetu vya chama ili utufafanulie zaidi mambo haya, hasa ni nani kakupa mamlaka ya kuthubutu kuyasema kwenye vyombo vya habari bila idhini ya chama. Taratibu zipo wazi, lazima zifuatwe.

(Mzee wa Lumumba)
 
Rais kasaini halafu kawaita wapinzani Ikulu, hawa wapinzani inabidi nao waangaliwe vizuri sasa, agenda yao tangu mwanzo ilikuwa rais kutosaini, sasa rais kasaini halafu kawaita Ikulu kunywa Juice na wao kama ilivyotarajiwa wakaenda.
Swali la kujiuliza kama rais alichagua kuwapuuza, je walienda kufanya nini? wanadhani itakuwa ni mwisho wa CCM kuendelea kutumia wingi wao? kila mtu anatambua kuwa kinachoshinda bungeni si hoja bali wingi.
Wapinzani wameandaliwa kifo chao kitaalam sana na wao wamekivaa kitanzi wakiamini kuwa ni tai. Na kuna kila dalili kuwa ni CCM yenyewe inayowapa nguvu wapinzani na muda wowote wanaweza kuziyeyusha nguvu zao hizo.
Walipewa nguvu lakini wao katika kuzitumia wamevuka mpaka, wawapao nguvu wamekasirika, wameamua kuagiza mtu wao mwingine atumie kete ya ukaguzi wa mahesabu which ipo obviously kuwa hawatachomoka.
Wameniudhi sana, acha tu yule aliyeingia akiwa na miaka 16 na sita awasambaratishe sasa....ili tuondokane na siasa hizi za vyama.
 
Back
Top Bottom