El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 297
- 537
Kwa malezi niliyoyapata toka kwa wazazi wangu na makuzi mengine katika maisha, huwa Sina kawaida ya kudharau mtu. Na naomba chapisho langu lisionekane kuwa personal na Mzee wassira bali litazamwe kama jicho la ukweli wangu.
Malezi hayo pia yamenifanya kuwa mkweli na mtu ambaye naweza kuongea mawazo yangu .
Kati ya mambo ambayo najua kwa hakika CCM wamejichanganya, ni kumtawadha mzee Stephen Masato wassira kuwa makamu mwenyekiti wa CCM.
Umri wake wa kuishi na umri aliokaa serikalini au ukipenda madarakani, tayari ni factors za kumfanya akose makali ya siasa na Uongozi wa wakati huu.
Tayari amezeeka kote ninavyomuona, kwenye siasa,( Hana, political metamorphosis) kama ulivyo umri wake ambalo ni jambo la kawaida la kibinadamu.
Mzee Joseph Sinde warioba , huyu ni mzee ambaye akili yake bado ni ya wakati huu hata kama ana uzee wa mwili. Kwa wassira ni tofauti sana, maana ni uzee kote.
Hakuna mahali unamuona mzee wassira, akiwa na toraha ya kisiasa ( political metamorphosis).
Mzee wassira hajataka kujibadilisha kabisa ( politically metamorphosized) Ili aendane na muda na wakati tulionao.
Ebu anza kuona anachofanya katika ziara zake. Anachoongea ni namna ya kubaki madarakani tu na hauoni mtu anayeongea mambo au issues za wakati na mambo yanayowasibu wananchi .
Haongei juu ya siasa za hoja na ushawishi ( influence), ingawa hii ni kama shida ya Wana CCM wote. Haongei juu ya issues zitakazoifanya nchi iendelee kistarabu ( Sophification),Bali mtu mmoja mbabe aliyepania kuwadogosha watu wanaotaka kunyemelea miliki yake. Anakosa high knowledge ya ukisasa wa mambo na nyakati hizi. Haongei juu ya watu kuwa huru katika nchi yao na real democracy ambayo ndo kiu ya watu wa nchi hii. Bado ana siasa za zamani za chama kimoja za ubabe na kuabudiwa.
Kwa wassira, sioni mwanasiasa wa nyakati hizi aliyejaa Sanaa ya siasa na siasa za kusaidia nchi kuwa na utulivu bayana, haki na demokrasia halisi. Mimi namuona mtu anayefanya siasa za zamani za madaraka na utukufu wa kulazimisha watu kuabudu chama tawala badala ya kuwashawishi watu kwa sera na kusambaza upendo. Huyu ni status quo politician.
Anazungumza mambo yaleyale ya miaka yote , ya kushika madaraka hata bila ushawishi, anaongea bila kuona Dunia inaelekea wapi, hata hajui anahudumia watu Gani wa wakati huu. He looks leading but out of hours. He is not a man of the hour, as I pointed out the other day on Freeman Mbowe. Na naona hapa mbele atawqpa wapinzani mileage ya kupata uungwaji mkono kama ataendelea na siasa zisizo za masuala na kuongea ukale ambao hauendani na nyakati hizi. ( Jambo ambalo najua haliwezi maana is mzee absolutely)
Ukimuona mwenyekiti wake, ambaye with due respect ambaye ni Rais wetu, unaona ile softness na adaptability ya new facts na anajua siasa za wakati huu zinataka Nini. Najua mtanipinga hapa, lakini tuwe wakweli, huyu Mzee wassira, anaweza kweli kuziona 4Rs kwa personality yake ngumu hivyo ya kisiasa?
Wengine mtasema 4Rs zimekwama, labda ni kweli zimekwama, lakini tuambiane ukweli, hivi kwa style ya maisha ya CCM na kwa muktadha wa hapa mzee wassira, hiyo falisafa ya Rais itatetewa na Hawa kina Mzee wassira ?
Soma Pia: Stephen Wasira amrithi Kinana nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara
Akina wassira wanajua madaraka tu na kwa aina yake amekuwa serikalini tangu miaka ya sabini, hivi huyu anajua shida halisi za watu? Huyu anajua wakati huu vijana ambao ni sehemu kubwa ya wananchi na nchi hii hawana ajira?
Akiwaona wanaandama kudai ajira, huyu kweli hataita polisi wawashughulikie badala ya kutafuta njia za kukutana na uhitaji wao?
Sijui CCM wanamuonaje, lakini frankly speaking, he is a man out of hours.
Let us think about this.