Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Baada ya CCM kumchagua ndugu Stephen Wassira kurithi kiti cha Kinana. Ameanza kutoa kauli ya kutaka kufanyakazi ya mwanzo kabisa ya maridhiano.....
CCM inadhani kuwa ikishakaa na CHADEMA wakaridhiana wanakuwa wameridhiana na taifa. Mimi nawakikisha Watanzania huru ambao hawaamini kwenye mbanga za wanasiasa kama mwatobaini pekee wa kero za nchi.
Mzee Wassira, haya ndiyo mambo muhimu ambayo CCM inapaswa kuzingatia kama inataka maridhiano
Ninachotaka kukuambia mzee Wassira na CCM
Hoja haijafungwa, hii ni hoja endelevu...
Wassira usidhani sisi ni watoto wadogo....
CCM inadhani kuwa ikishakaa na CHADEMA wakaridhiana wanakuwa wameridhiana na taifa. Mimi nawakikisha Watanzania huru ambao hawaamini kwenye mbanga za wanasiasa kama mwatobaini pekee wa kero za nchi.
Mzee Wassira, haya ndiyo mambo muhimu ambayo CCM inapaswa kuzingatia kama inataka maridhiano
- Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 8 inatamka wazi kuwa serikali inapata mamlaka yake kutoka kwa wananchi. Katiba imetoa mwongozo wa namna wananchi wanavyochagua viongozi. Hivyo kuridhiana na vyama vya kisiasa pakee ni uhuni na kuwadharau Watanzania
- Tangu tumeingia siasa za vyama vingi, wananchi wametendewa makosa makubwa na mengi ambayo yamesababishwa na NIA, UCHU na DHAMIRA mbaya ya CCM kujimilikisha nchi kinyume na misingi ya Uhuru wa Tanganyika. Mambo hayo yapo kwenye sheria mbalimbali za kikatili na za hovyo ambazo zinapingana na Katiba iliyopo. Sheria ya Tume ya Uchaguzi. Sheria ya TAMISEMI, Sheria ya Polisi, Sheria ya vyama vya siasa na sheria zinazofanania. Ibara ya 18 ya Katiba imetungiwa sheria kinzani kuzuia haki hizo za kikatiba
- CCM imekuwa ikiahirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama wakiwemo Polisi, na Usalama wa Taifa kukandamiza na kubaka michakato yote ya kidemokrasia nchini. Wizi wa Kura na matendo maovu ya uchaguzi yanahitaji maridhiano ya kitaifa
- Matukio ya utekaji nyara, uteswaji na mauaji dhidi ya raia wa Tanzania pamoja na wanasiasa wa CHADEMA yamekuwa yakichochewa na kauli za viongozi wa CCMna kutekelezwa na vyombo vya dola. Na kauli za Amiri Jeshi Mkuu kuwa matumio hauo ni drama na kutochukua hatua.... National Reconciliation haikwepeki hapo
- Mikataba mibovu inayoweka mazingira ya wizi wa rasilimali zetu na ugenishaji wa vyanzo vyetu vikuu vya mapato, hawajakosewa CHADEMA pekee bali sisi Watanzania
- Mihimili ya Serikali ambayo ni Bunge na Mahakama kuungana na Executives kukandamiza taifa na kuchezea michakato ya utoaji haki the only thing needed ni Maridhiano ya Kitaifa
- Mambo ni mengi na ninaamini great thinkers wenzangu wataongezea mengine
Ninachotaka kukuambia mzee Wassira na CCM
- CCM iliombe radhi Taifa kwa matendo yote maovu dhidi ya Taifa
- CCM ijiandae kushirikiana na Wananchi kwenye mchakato wa Katiba Mpya kabla ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025
- CCM itamke hadharani na mpaka kwenye majukwaa ya kimataifa kuwa ipo tayari kukabidhi madaraka kwa mshindi halali wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baada ya kupata Katiba Mpya.
Hoja haijafungwa, hii ni hoja endelevu...
Wassira usidhani sisi ni watoto wadogo....