Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,860
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira amesema ni vyema Watanzania wakafikiria kudumisha Muungano kwa kutazama kero zilizoonekana miaka 50 iliyopita ikiwemo kero za watendaji, sheria na kuondoa kabisa kero zote ili kuweza kusonga mbele.
Aidha alisema serikali mbili bado zinafaa zaidi kwani kuwa na serikali tatu kutakuwa ni gharama zaidi kuendesha nchi. Kauli hiyo aliitoa juzi wakati wa mahojiano mjini hapa kuhusu masuala mbalimbali yanayokabili taifa kwa sasa, ikiwamo mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba.
"Kuna mambo makubwa zaidi ambayo bunge hili linatakiwa kuamua kuliko hili la serikali mbili, kufikiria kuwa na serikali tatu utalipa gharama kubwa zaidi," alisema.
‪source: clouds radio