Wastaafu kufanya matembezi kuchangisha fedha za wakili

Wastaafu kufanya matembezi kuchangisha fedha za wakili

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Wastaafu kufanya matembezi kuchangisha fedha za wakili
Na Fidelis Butahe

BAADA kufunguliwa kesi mahakamani na serikali kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali, wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameazimia kufanya matembezi ya hiari kuchangisha fedha za kuwawezesha kuweka mawakili wa kuwatetea.


Jumatano wiki hii wastaafu nane wa EAC akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Nathaniel Mlaki walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali hali na kusababisha msongamano mkubwa wa magari jijini Dar es Salaam.


Wastaafu hao ambao waliazimia kuandamana mpaka ubalozi wa Uingereza walikatikasha safari yao baada ya kuzingirwa na polisi katika makutano ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Umoja wa mataifa ambapo walikaa katika kati ka kusababisha msongamano wa magari sehemu zote za barabara hizo.


Baada ya juhudi za polisi kuwaondoa kwa amani kushindikana, walitumia nguvu pamoja na kisha kuwakamata viongozi wao wakawapeleka Kituo Kikuu cha Polisi na kisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Akizungumza na waandishi wa habari jana Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee wa Afrika Mashariki, Nathaniel Mlaki alisema wameamua kufanya matembezi hayo ili kuweza kupata wahisani wa kuwachangia fedha za kuwalipa mawakili watakaowatetea makahamani dhidi ya kesi inayowakabili.


"Pamoja na haya yote pia tunatarajia fedha tutakazo pata katika matembezi haya zitatusaidia kutatua matatizo madogomadogo yanayowakabili wazee wa EAC waliotoka mikoani ambao wapo jijini kwa zaidi ya miaka miwili," alisema Mlaki na kuongeza:


"Matembezi haya tunatarajia kuwashirikisha wafanyabiashara, viongozi wa dini mbalimbali, wanasiasa, vyama vya siasa, watu maarufu, mashirika ya haki za binadamu, taasisi binafsi na wananchi ambao hawafahamu madai yetu ili tuwaeleze juu ya tunachokidai, maana serikali imekuwa ikiwadanganya".


Alisema pamoja na matembezi hayo ya hiari azma yao ya kuandamana nchi nzima bado iko palepale kama serikali haitakuwa tayari kukaa nao mapema ili kulipatia ufumbuzi tatizo la malipo yao.


Aidha alisema kilio chao kikubwa ni kuitaka serikali ikubali kukaa na kamati yao ili kuweza kukokotoa kwa pamoja malipo ya wastaafu kwani hesabu za malipo zilizofanywa na serikali ni za mwaka 1948 na kwamba hazipo katika mkataba ulioletwa na mpatanishi aliyekuja kugawa mali za EAC kwa amani na usawa baada ya kuvunjika Juni 30, 1977, Dr Victor Umbritch kutoka uswisi.


Alisema mpatanishi huyo alikamilisha ripoti yake ya mwanzo Oktoba 28,1981, ripoti ambayo ilitoa nyaraka muhimu za mgawanyo wa mali za iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Aidha baada ya kukamilika kwa mambo yote mpatanishi huyo alikabidhi kila kitu kwa serikali hizi tatu hapo ndio serikali hizi tatu zilitiliana saini ya makubaliano ya mgawo zikiwamo za mafao ya waliokuwa wafanyakazi wa jumuiya hiyo.


Alisema fedha hizo ziligawanywa katika mafungu matatu ambapo Kenya walipewa asilimia 42, Tanzania asilimia 32 na Uganda 26
 
Back
Top Bottom