Leo ilikuwa ni siku ya Wafanyakazi dunia nzima. Hapa Tanzania sherehe hii iliadhimishwa Mjini Morogoro na mgeni rasmi alikuwa Mhe. Samia Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Sherehe kama ya leo ndiyo wafanyakazi wanawasilisha kero zao mbele ya Mgeni Rasmi ili zifanyiwe kazi. Sisi Wastaafu tuna kero nyingi sana lakini hatuna nafasi ya kukutana na Mhe. Rais ili tuziwasilishe kwake. Mojawapo ya kero zetu ni Pensheni ndogo tunayopata.
Kutokana na kupanda kwa maisha Wastaafu wanatakiwa kufikiriwa ili pensheni zao ziweze kurekebishwa. Aliyekuwa Rais wa Awamu ya nne aliweza kuturekebishia kidogo pensheni zetu lakini mpaka leo hakuna kilichofanyika.
Mhe Rais sisi Wastaafu tunaishi maisha magumu sana tunakuomba sana utufikirie kwa kuongeza kiwango cha pensheni zetu. Tumetumikia nchi hii. Tumeikosea nini Serikali?