Wastaafu waangua kilio kwa kufukuzwa na kufungiwa geti, nyumba za TBA

Wastaafu waangua kilio kwa kufukuzwa na kufungiwa geti, nyumba za TBA

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Familia mbili za Wastaafu wa serikalini ambao walikuwa wakiishi katika nyumba za Wakala wa majengo (TBA) jijini Arusha wanakumbwa na hali ya sintofahamu baada shirika hilo kuwafurusha kwa kutoa vitu vyao nje kwa madai ya kushindwa kulipa kodi.

Familia hizo zinadai ni takribani mwezi mmoja sasa wanalala nje huku vitu vyao vikiwa vimezuiwa na Mamlaka hiyo.

Wapangaji hoa walikuwa watumishi wa shirika la taifa la Usagaji Nafaka na sasa wanasema vitu kama vile vitanda, televisheni, majiko, na kuachwa nje ya nyumba hizo vikiendela kuharibika.

Kwa sasa hawawezi kuingia katika nyumba hizo baada ya ya geti kufungwa.

Wameomba msaada kutoka mamlaka za juu ikiweno ya Rais kuangalia namna wanavyoweza kusaidika

Akiongea kwa njia ya simu Meneja wa TBA Mkoa wa Arusha Steven Simba amesema sababu kubwa za kuwatoa wapangaji hao ni kutokana na malimbikizo ya kodi, ambazo wapangaji hao wamekuwa wakikwepa kuzilipa.
 
Toka dunia iumbwe sheria ya deni ni kulilipa tu, sio kuomba siasa
 
Back
Top Bottom