Wastaafu walipwe pensheni yote kwa mkupuo ndani ya mwaka mmoja baada ya kustaafu

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kwanini wastaafu huwa wanendelea kulipwa kila mwezi pesa kidogo kidogo baada kupewa kwa mkupuo kiasi kikubwa pindi wanapostaafu badala ya kupewa pesa zao zote ndani ya muda mfupi wa kustaafu kwao?

Hizi pesa za pensheni wanazopewa kila mwezi ni za kuganga njaa tu na huwa hawewezi kudunduliza kufanyia nazo mambo makubwa ya maendeleo pia ni kupoteza muda na kuingezea serikali mzigo usiokuwa wa lazima wa kusimamia na kufuatilia kila siku mafao ya hawa wazee wastaafu.

Ni vyema serikali ikawa inawapa pesa zao zote angalau ndani ya mwaka mmoja baada ya kustaafu ili huyo mstaafu mwenyewe akajue pa kuzipeleka ua jinsi ya kuzitumia.
 
"KUWA UYAONE"
NDIO MAANA YA KUITWA MAFAO YA UZEENI; ILI KUMSAIDIA MZEE AWEZE KUISHI BILA KUWA TEGEMEZI KATIKA JAMII BAADA YA KUSTAAFU.
 
Hao ni watu wazima, waache waishie pabaya.
Kama tuliwaamini kwenye utumishi wa umma kwa miaka 30 tunashindwa vipi kuwaamini ku manage vijisenti vyao vya pensheni.
Hayajakukuta ww bora hvyo kidogo kidogo kuliko hivyo unavyotaka ww wataishia pabaya
 
Wastaafu wenyewe wanapenda hivyo. Pesa nyingi kwa mkupuo mmoja ni kutafuta mauaji ya presha kutokana na kudhulumiwa,kutapeliwa ,kuvamiwa etc
 
Mtu wa miaka 55 anashindwa vipi kutunza na kutumia pesa zake hadi ahitaji kuangaliwa kama mtoto mdogo?

Wengi wameshazoea kulipwa kidogo kidogo sasa akilipwa kwa mkupuo kinakuja kiwewe cha matumizi hapo ndipo wanapoibuka wapambe,ndugu ,jamaa na marafiki kila mmoja akitoa wazo lake. mwisho wa siku mstaafu anaishia kufulia vibaya mno

Mkuu, kama mkupuo jumla ni milioni 70 mstaafu atakuwa anapewa bei gani kila mwezi?
 
Hayajakukuta ww bora hvyo kidogo kidogo kuliko hivyo unavyotaka ww wataishia pabaya
Wataishia kubaya ni wewe umeagiza. Wabunge wazee wanapolipwa kwa mkupuo wangapi wameishia kubaya. Kila mtu na akili yake.
 
Mtoa mada unajua kwamba mafao TZ yanatolewa kama bima (kwa kutumia kikokotoo) na siyo kama akiba (ulichoweka ndicho unachopewa)? Unajua kikokotoo kinatema pesa nyingi kuliko mtu angalipewa kile tu alichochangia (hata ungijumlisha na kiasi kidogo cha riba)?

Ukisema "apewe zote" --- zipi? Michango yake (midogo kuliko jumla kuu ya kikokotoo). Dhana ya pensheni kama bima ni kitu muhimu.

Cha msingi kile kiinua-mgongo kisichelewe, na pensheni ya kila mwezi halikadhalika.

Hao ni watu wazima, waache waishie pabaya.
Kama tuliwaamini kwenye utumishi wa umma kwa miaka 30 tunashindwa vipi kuwaamini ku manage vijisenti vyao vya pensheni.
Usiseme hivyo, angalia asilimia kubwa ya wastaafu hawana uwezo au maarifa ya kuweka akiba wakati wa ujana wao, hivyo hizo unazoziona wewe ndogo ndizo zinazotusaidia uzeeni.

Aidha baadhi ya nyinyi vijana pia munatuwacha wazee bila ya msaada wowote baada ya kutumia fedha zetu nyingi kuwasomesha na kuwahudumia nyinyi.

Tuwacheni jamani.
 
Mtu wa miaka 55 anashindwa vipi kutunza na kutumia pesa zake hadi ahitaji kuangaliwa kama mtoto mdogo?
He wewe unatoka dunia gani, hii hii tunayoishi sisi wengine?

Kua uyaone baba usifanye haraka.
 
Kwanini wastaafu huwa wanendelea kulipwa kila mwezi pesa kidogo kidogo baada kupewa kwa mkupuo kiasi kikubwa pindi wanapostaafu badala ya kupewa pesa zao zote ndani ya muda mfupi wa kustaafu kwao?
Kuna Pension ya kila mwezi na Kiinua Mgongo ambacho anapewa kwa mkupuo
Hizi pesa za pensheni wanazopewa kila mwezi ni za kuganga njaa tu na huwa hawewezi kudunduliza kufanyia nazo mambo makubwa ya maendeleo
Naam hio ndio maana ya pension.., kuganga njaa ili mtu huyu aliyezeeka na sasa hana nguvu kama zamani asiwe mzigo kwa jamii..., unataka afanye mambo makubwa ya maendeleo yapi ambayo hakufanya maisha yake yote...., hapa ni kulia kivulini kile alichochumia juani enzi za ujana wake
pia ni kupoteza muda na kuingezea serikali mzigo usiokuwa wa lazima wa kusimamia na kufuatilia kila siku mafao ya hawa wazee wastaafu.
Hapana hao ndio kazi zao kuhakikisha wanakusanya pesa za wachangiaji na kuwapa wale wazee waliostaafu mpaka siku wakifa
Ni vyema serikali ikawa inawapa pesa zao zote angalau ndani ya mwaka mmoja baada ya kustaafu ili huyo mstaafu mwenyewe akajue pa kuzipeleka ua jinsi ya kuzitumia.
Iwape pesa zao kwa mkupuo alafu siku zikiisha waanze kuwa omba omba mitaani ambapo jamii iingie tena mfukoni kuwalea, au unataka wawe omba omba uzeeni ?
 
Wakishapewa hizo hela waje mtaani tuwafundishe siri ya utajiri iliyopo kwenye forexi na biashara za kimtandao kama Q-neti ili tuwe na wastaafu wengi mabilionea🤣🤸🐒
 
Kwanini wastaafu huwa wanendelea kulipwa kila mwezi pesa kidogo kidogo baada kupewa kwa mkupuo kiasi kikubwa pindi wanapostaafu badala ya kupewa pesa zao zote ndani ya muda mfupi wa kustaafu kwao?

Hizi pesa za pensheni wanazopewa kila mwezi ni za kuganga njaa tu na huwa hawewezi kudunduliza kufanyia nazo mambo makubwa ya maendeleo pia ni kupoteza muda na kuingezea serikali mzigo usiokuwa wa lazima wa kusimamia na kufuatilia kila siku mafao ya hawa wazee wastaafu.

Ni vyema serikali ikawa inawapa pesa zao zote angalau ndani ya mwaka mmoja baada ya kustaafu ili huyo mstaafu mwenyewe akajue pa kuzipeleka ua jinsi ya kuzitumia.
Subiri mda wako wa kustaafu ndipo tuombe hivyo.
 
Back
Top Bottom