Wastaafu walipwe pensheni yote kwa mkupuo ndani ya mwaka mmoja baada ya kustaafu

Kile wafanyakazi wanachochangia kwenye hiyo mifuko huwa kinawekezwa na kuzalisha kingi zaidi kwa takribani miaka 30. Huenda kungekwa na mifuko binafsi ya pensheni yenye ushindani wangelipwa kingi zaidi.
 
Hiyo pensheni ya kila mwezi ichanganywe yote kwa pamoja na kiinua mgongo mstaafu alipwe kwa mkupuo.

Serikali iuze hisa kwa wafanyakazi wastaafu kwa mashirika kama NHC, bwawa la Umeme la Nyerere na mengineyo hizo pesa zao zizungushwe zizalishe zaidi badala ya kuchota tu kodi za wananchi muda wote kugawia hao wazee.
 
Kwani Infantry Soldier anasemaje kwenye hii issue?
 
Hiyo pensheni ya kila mwezi ichanganywe yote kwa pamoja na kiinua mgongo mstaafu alipwe kwa mkupuo.
Akilipwa kwa mkupuo akizila zote na kuwa omba omba uzeeni ni mzigo kwa jamii
Serikali iuze hisa kwa wafanyakazi wastaafu kwa mashirika kama NHC, bwawa la Umeme la Nyerere na mengineyo hizo pesa zao zizungushwe zizalishe zaidi badala ya kuchota tu kodi za wananchi muda wote kugawia hao wazee.
Pension funds ndio inachokifanya theoretically..., inachukua pesa za wachangiaji (sio kodi) mwajiriwa anakatwa na mwajiri anamuongezea mwajiriwa na pesa kupelekwa kwenye pension funds ambazo inazizungusha ili mfuko usifilisike..., kwahio practically wanaowaweka wazee mjini ni wachangiaji wa sasa..., tatizo kama hili ndio liliwapata Japan kutokana na kwamba wazee ni wengi hence wachangiaji wanapungua kuliko wachangiwaji (old people population increasing)
 
Wakishapewa hizo hela waje mtaani tuwafundishe siri ya utajiri iliyopo kwenye forexi na biashara za kimtandao kama Q-neti ili tuwe na wastaafu wengi mabilionea🤣🤸🐒
Munazisubiri kuzifanyia utapeli, na hayo ndiyo yanayowafika wazee wengi huku kwetu, hasa kwa vile hawajawahi kupata fedha nyingi kwa mkupuo kwa hivyo zinawachanganya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…