Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mjomba masomo ya kid2 yanatakiwa yawe 9 au zaidi,hivyo ombi lako liko kinyume na sera ya elimu,kwa ushauri kama unapenda masomo machache nenda kasomee QT.Wastani wa kufaulu kidato cha 2 uzingatie idadi ya masomo wanayofundishwa wanafunz ktk shule husika e.g: 5, 6, 7, 8 au 9
Sera ya elimu ya Tanzania inazitaka shule za secondary kufundisha masomo ya lazima tisa, kinyume na hapo ni uvunjifu wa sheria.Wastani wa kufaulu kidato cha 2 uzingatie idadi ya masomo wanayofundishwa wanafunz ktk shule husika e.g: 5, 6, 7, 8 au 9
Ni kweli kuna shule za kata zenye walimu wawili (2) tu. Lakini walimu hao ni wale wa kuajiriwa na serikali. Pamoja nao unakuta walimu wa part time ambao kati yao ni form six leavers na wengine huwa ni diploma holders wanaongoja ajira na wakati mwingine walimu huazimwa toka shule ya jirani. Mara nyingi wakuu wa shule hutumia busara za kuajiri hao walimu wa muda ili watoto wafundishwe masomo 9 ambayo ni History, Civics, Geography, English, Kiswahili, Basic Maths, Biology, Chemistry na Physics. Masomo hayo ndiyo 'basic' kwa kidato cha kwanza na cha pili na mwongozo unaoelekeza hivyo upo. Hata ukisikia shule ina walimu 2 chunguza utakuta kuwa masomo hayo 9 yanafundishwa kwa kutumia walimu nilioeleza hapo juu. Na uelewe kuwa mtihani wa kidato cha 4 mwanafunzi anatakiwa afanye masomo si chini ya 7 ili aweze kupewa daraja analostahili. Mwanafunzi anasoma masomo 9 au zaidi awapo kidato cha 1 na 2 ili awe na uwanja mpana wa kuchagua 'combinations' 5 anazomudu akiingia kidato cha 3 na hatimaye kidato cha 4. Sasa wewe unapotaka kidato cha pili wapewe wastani kutokana na masomo aliyofanya hata kama ni 5 au 6 huoni kuwa mwanafunzi atakwama huko mbele ya safari? Atakuwa hana uchaguzi. Hoja yako haina mashiko. Ungejadili na kupinga kwa nini shule za kata zinaingizwa kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta 'top ten schools' katika mtihani wa kidato cha 4 huku zikichanganywa na shule za seminari au zile za vipaji maalumu hapo ndo nitakuelewa.Hujanielewa. Hivi mkoani kwako hakuna shule za kata zenye walimu wa2? Unawasaidiaje wanafunzi wa shule hizo?
Umeona eh? Tena walisema elimu itakuwa bure toka chekechea hadi chuo kikuu. Hoyeee CCM kwa kuanzisha sekondari lukuki kama nyuki. Hoyeee CDM (2015) kwa sababu mtapeleka watoto lukuki chuo kikuu bure. HOYEEE WOTE.Kuongeza shule ni sera ya ccm,elimu bora ni sera ya chadema hvyo ccm kazi yao wamemaliza safi,tunawaomba wananchi wajiandae kutoa kura za kutosha kwa cdm hili kusimamia sera hiyo,namunukuu mh Mbowe mwenyekiti wa chama na msemaji mkuu wa kambi rasimi bungeni,CDM TUKIINGIA MADARAKANI SERA YETU YA KWANZA NI ELIMU,YA PILI ELIMU YA TATU ELIMU,