Wastani wa Umri wa Kuishi Umeongezeka hadi Miaka 66

Wastani wa Umri wa Kuishi Umeongezeka hadi Miaka 66

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Akizungumza jijini Arusha Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais- Uwekezaji na Mipango Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa Wanawake wanaishi umri mkubwa wa zaidi ya miaka 68 ikilinganishwa na Wanaume wanaoishi miaka 64

“Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022 imeonyesha kuwa umri wa Mtanzania kuishi sasa ni miaka 66, ikimaanisha wastani wa kuishi umeongezeka kwa miaka 14 ukilinganisha na mwaka 2000 ambapo wastani wa kuishi ulikuwa ni miaka 52” amesema

Amesema hii ni miongoni mwa mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Dira ya maendeleo ya mwaka 2000/2025 huku lengo lilikuwa ifikapo 2025 umri ufikie miaka 68.
 
Back
Top Bottom