Wastara amchimba mkwara mpenzi wake, Bond

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506

Msanii wa bongo movie Wastara amemchana mpenzi wake wa sasa Bond kwamba asipojirekebisha baadhi ya tabia zake atamuacha na akimwacha hatarudi tena kwake.

Hata hivyo Wastara amesema anaweza kuvumilia shida anazopata kwa Bond lakini anaweza kumuacha muda wowote kwani hahitaji ‘stress’ za kimapenzi huku akiweka wazi kuwa amejitahidi na amefanikiwa kumrekebisha kwa 80 % na endapo ataendelea na mambo yake ya zamani zamani ataachana naye.

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Wastara amesema “Niseme tu ukweli kwamba kwa Sajuki hakuna mtu anayeweza kufikia upendo wetu kwa kuwa Sajuki alikuwa anajali kila kitu ambacho nilikuwa nakipenda, kitu ambacho mpaka sasa sijapata ni mtu ambaye amefikia hatua za Sajuki “. Alisema Wastara.

Source: Eatv.
 
huyu mwanamke ana mapepo ama amnataka kuwa juu ya mwanaume ...... kila muda kuachana tu

ama akishalichoka dushe anaanza kelele............
 
Kitu asichokijua wastara ni hakuna mkamilifu 100% zaidi ya aliye juu

Amuache aende kwa mwingine ambaye naye atakuwa na mapungufu
Mwisho wa siku ndio inafikia ile stage ya mwanamke 'screpa'
 
Kitu asichokijua wastara ni hakuna mkamilifu 100% zaidi ya aliye juu

Amuache aende kwa mwingine ambaye naye atakuwa na mapungufu
Mwisho wa siku ndio inafikia ile stage ya mwanamke 'screpa'
Asepe tu moja kwa moja ili na mimi nitege mingoo maana ashakuwa cha wote
 
huyu si aliolewa na mbunge huko zenji..
 
Hivi, inakuwaje mwanamke anakutawala?!
 
Hivi huyu kwanini anapenda kututangazia sisi maisha yake ya kimapenzi yasiyodumu??!!
 
Kitu asichokijua wastara ni hakuna mkamilifu 100% zaidi ya aliye juu

Amuache aende kwa mwingine ambaye naye atakuwa na mapungufu
Mwisho wa siku ndio inafikia ile stage ya mwanamke 'screpa'
Lait angekusikia
 
Kitu asichokijua wastara ni hakuna mkamilifu 100% zaidi ya aliye juu

Amuache aende kwa mwingine ambaye naye atakuwa na mapungufu
Mwisho wa siku ndio inafikia ile stage ya mwanamke 'screpa'
wanaume wote wako kama wamezaliwa na mama mmoja tabia zao hazitofautiani sana
 
Ujumbe kwa wastara. Sio kila kitu maishani mwako ni cha kukianika hadharani,vingine avifukie moyoni.
 
Eti useme mpenzi wako wa zamani alikuwa bora zaidi ya mm wa sasa...utaisoma no hapohapo huyu bond nae labda mario
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…