Wastara asaini mkataba mnono wa zaidi ya Tshs Milioni 400

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Malkia wa filamu Wastara Juma amepata shavu la kuwa balozi wa kampuni ya simu za mkononi ya KZG Tanzania yenye makao makuu yake nchini China.

Katika mkataba huo mwigizaji huyo atavuna kiasi cha tsh milioni 400 kwa miaka miwili akiwa balozi wa kampuni hiyo kwa matangazo na matamasha mbalimbali.

Akiongea na Filamu Central meneja mauzo wa kampuni ya KZG Tanzania, Raymond Kalikawe amesema kuwa kamapuni yao imelenga kusambaza teknolojia vyuoni kwani wana bidhaa nyingi ambazo zinatumika katika kufundishia wanafunzi hao.

“Leo pia tunazindua simu ya kipekee kabisa kufika hapa nchini Kzg Kimi ambayo inatumia betri ya ndani kwa ndani ambayo ina sifa ya kutengenezeka tofauti na zingine ambazo betri zake zikiharibika hazitengenezeki,”alisema Kalikawe.

Pia Wastara ameishukru kampuni hiyo kwa kumwamini na kutambua kuwa ana vigezo stahili kuwa balozi wao na kuahidi kuwa hatowaangusha katika kuitangaza kampuni hiyo sambamba na bidhaa zake zilizalishwazo na kampuni hiyo ambayo utengeneza simu, Computer na vifaa vingine vya teknolojia.

Uzinduzi huo ulisindikizwa na wasanii wa Bongo movie wakimpongeza Wastara kuingia mkataba huo.
 
Safi sana wastara, sasa utatulia ulee wanao maana kwa mheshimiwa ulidhalilika sana, pesa zilikupeleka kule ukaambulia kashfa., kazi yako ndio silaha bora mama piga kazi lea wanao katika njia nzuri nao hawataiacha hata watakapokuwa wazee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…